WAHITIMU TAALUMA YA UREKEBISHAJI WASHAURIWA KUTUMIA VIZURI ELIMU WALIYOIPATA.

Subscribe Us

WAHITIMU TAALUMA YA UREKEBISHAJI WASHAURIWA KUTUMIA VIZURI ELIMU WALIYOIPATA.

Na. Javius Byarushengo na Mawazo Mtondo - DSM. 
------------------------------------------------------------

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Daniel Baran Sillo (mb), amesema kuwa anayo faraja kuona Jeshi la Magereza linaendelea kupata wataalamu watakaokabiliana na uhalifu mamboleo katika Dunia ya sasa inayokua kwa kasi katika nyanja za Sayansi na Teknolojia.

Kauli hiyo ameitoa leo Novemba 15, 2024 katika mahafali ya pili ya kozi ya Stashahada ya Sayansi ya Urekebishaji, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Cha Taaluma ya Sayansi ya Urekebishaji Ukonga jijini Dar es Salaam. 

Aidha Mhe. Sillo amewataka wahitimu hao kutumia maarifa waliyopata chuoni hapo kuleta matokeo chanya katika taasisi, huku akimpongeza Kamishna Jenerali wa Jeshi la  Magereza Jeremiah Katungu na uongozi wa Chuo kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya Chuo hicho.

Awali Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Jeremiah Yoram Katungu, akimkaribisha Mhe. Naibu Waziri amemshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Magereza ili litimize majukumu yake,huku akitoa rai kwa wahitimu na kusema kuwaJeshi na Serikali lina matarajio makubwa na wao katika kuleta ufanisi maeneo ya kazi. 

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe. Edward Jonas Mpogolo akitoa salaam amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kujenga  Hospitali ya kisasa inayomilikiwa na Jeshi la Magereza iliyopo Ukonga ambayo inahudumia Askari, Wafungwa pamoja na jamii inayoizunguka. 
 
Naye Mwenyekiti wa bodi ya Chuo Dkt. Zena Mabeyo amewasii wahitimu kutobweteka baada ya kuhitimu elimu waliyoipata. 

Katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 47 wamehitimu kati yao wanawake 14 na wanaume 33 ambapo Viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali walihudhuria.

(Picha na.A/Insp.  Nurdin Nanyanga  na Cpl John Mandago) 

Post a Comment

0 Comments