WANAMUZIKI WANAWAKE ARUSHA WAPIGA KAMBI KUANDAA WIMBO MAALUMU WA MAADHIMISHO YAO MACHI NANE - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, February 28, 2025

WANAMUZIKI WANAWAKE ARUSHA WAPIGA KAMBI KUANDAA WIMBO MAALUMU WA MAADHIMISHO YAO MACHI NANE



Katibu Mkuu wa Tanzania Music Foundation  (TAMUFO) Stella Joel  

Mwanamuziki Maarufu Dipper Rato


Na Dotto Mwaibale

Wanamuziki wanawake wa Mkoa wa Arusha kuyapamba Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani Ambayo Kitaifa Yatafanyika Mkoa wa Arusha Kilele cha Maadhimisho hayo ni Tarehe 8Machi 2025 Katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mgeni Rasmi ni Mheshimiwa Dr Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza na Waandishi wa Habari,  Katibu Mkuu wa Tanzania Music Foundation  (TAMUFO) Stella Joel alisema Katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Wanamuziki Wanawake Wa Mkoa Wa Arusha Arusha Women Stars Wamerekodi Wimbo Maalum Uliobeba Ujumbe wa Kauli Mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani 2025.

Alisema wimbo huo mahususi kwenye maadhimisho hayo umelenga kuunga mkono jitihada mbalimbali za Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Mwanamuziki Maarufu Dipper Rato alisema wimbo huo umeisha kamilika tna kuwa ayari  wakati wowote utaanza kusikika kwenye media mbalimbaliVyombo vya Habari.

“ Tunamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwa Kuutambua Mchango wa Wanamuziki katika Maendeleo ya Nchi Yetu na kuweza kuhamasisha makundi mbalimbali ya Mkoa wa Arusha kushiriki shughuli  za maendeleo.

Baadhi ya Wanamuziki Wanawake wa Mkoa wa Arusha wameamua kurekodi nyimbo mbalimbali za kuhamasisha  Wanachi kudumisha Amani na Utulivu katika nchi yetu pamoja na kuhamasisha maendeleo katika Jamii na kulinda Heshima ya Muziki na utamaduni wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad