OCD Awadhi Chico enzi za uhai wake.
....................................................
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake
wamejitokeza kwa wingi katika mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya
Kipolisi ya Chanika, Kamishna wa Operesheni ya Mafunzo Tanzania (CP) Awadhi Chico.
CP Awadhi Chico alifariki saa 1: 20 asubuhi Machi 17, 2025
katika ajali ya gari iliyohusisha daladala eneo la Pugu mwisho wa lami jijini
Dar es Salaam ambalo liliacha njia na kwenda kuparamia gari dogo aina ya Prado
lilokuwa likiendesha na OCD huyo na kufariki papo hapo huku mtu mwingine
aliyekuwemo kwenye gari hilo akijeruhiwa.
Mazishi ya OCD Chico yamefanyika Machi 18, 2025 katika
makaburi ya Kisutu huku baadhi ya waombolezaji wakimzungumzia kwa mambo mema
aliyokuwa akiyafanya na kumuelezea kuwa alikuwa mtu wa watu.
OCD Chico baba yake alikuwa ni Kamanda wa Polisi katika
baadhi ya mikoa hapa nchini na kuwa wakina Chico ni watoto wazawa wa Kariakoo
jijini Dar es Salaam.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa tayari kwa mazishi ya OCD Awadhi Chico.
Waombolezaji wakiwa kwenye shughuli hiyo ya maziko.
Viongozi mbalimbali na viongozi wa dini ya kiislamu wakiwa kwenye maziko.
Dua la kumuombea marehemu Chico ikifanyika.

















No comments:
Post a Comment