RAIS SAMIA AZINDUA MRADI WA MAJI SAME-MWANGA-KOROGWE - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, 9 March 2025

RAIS SAMIA AZINDUA MRADI WA MAJI SAME-MWANGA-KOROGWE

Muonekano wa mradi wa maji uliozinduliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Same-Mwanga-Korogwe mkoani Tanga na Kilimanjaro.

..........................................

Na Mwandishi Wetu, Tanga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo amezindua rasmi Mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe, akiwataka wananchi kuunganisha huduma ya maji, kulipa bili kwa wakati, na kutunza miundombinu ili kuhakikisha mradi huo unadumu kwa muda mrefu.

Akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro katika viwanja vya CD Msuya Wilayani Mwanga, Rais Dkt. Samia amesema serikali itaendelea kuwekeza katika miradi ya maji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma safi na salama. Ameongeza kuwa maji ni nyenzo muhimu ya maendeleo, hivyo kila mmoja anapaswa kuwa sehemu ya ulinzi wa miundombinu ya mradi huo. 

Kwa upande wake, Waziri wa Maji Jumaa Aweso amempongeza Rais Samia kwa dhamira yake ya dhati ya kutatua changamoto za upatikanaji wa maji nchini. Ameeleza kuwa mradi huo umetekelezwa kwa ufanisi mkubwa, huku akiwashukuru wadau, watendaji na wasimamizi wa mradi kwa juhudi zao kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amesema mradi huu utakuwa suluhisho la muda mrefu kwa wananchi wa maeneo husika ambao walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji.

Muonekano wa mradi huo.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiangalia mradi huo.

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad