TAASISI YA RAMADHANI CHARITY YATOA SADAKA YA IFTAR MISIKITINI, KADHI KAOJA ATOA NENO - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, 22 March 2025

TAASISI YA RAMADHANI CHARITY YATOA SADAKA YA IFTAR MISIKITINI, KADHI KAOJA ATOA NENO

KADHI wa Mkoa wa Singida, Shekhe Ramadhani Kaoja, amewataka wananchi kujenga tabia ya kutoa sadaka ya iftar kwa watu waliofunga katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani  ili waweze kuvuna dhawabu kwa mwenyezi Mungu.

Alisema hayo juzi wakati wa kutoa sadaka ya iftar kwa wananchi katika miskiti mitatu  iliyopo wilayani Ikungi ambayo ilitolewa na Taasisi ya Ramadhani Charity Program 2025 chini ya Mwenyekiti Ahmed Misanga.

Shekhe kaoja  alisema wananchi lazima watambue kuwa kuwajali watu wenye mahitaji na misikini ni jambo jambo ambalo linampendeza mwenyezi Mungu kwa kuwa hata mitume walifanyia wema watu masikini.

"Napenda kutoa rai kwa waumini wenzangu tupende kutoa faraja na Sadaka ya Iftar kwa makundi kama haya hasa katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani kwani Allah anapenda watu ambao wanatoa swadaka," alisema Kaoja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Ramadhan Charity Program 2025, Ahmed Misanga, alisema wamemua kushirikiana na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida kutoa sadaka iftar hiyo kwa ajili ya jamii yenye uhitaji  iliwaweze kupata dauku na futari katika kumi la mwisho la Ramadhani.

Leo tumetembele misikiti ya Mwaru, Mpunguzi na msikiti wa Sepuka na kutoa swadaka zetu kwa pamoja na Ofisi ya Kadhi wa Mkoa wa Singida,tunamini kupitia swadaka hii tumewagusa moja kwa moja watu wenye uhitaji katika hili kumi la mwisho la Ramadhani," alisema Misanga.

Aidha, Misanga aliwaomba Watanzanai  wenye uwezo kutoa swadaka basi watoe kwani swadaka inaondoa balaa na vifungo na kufungua neema kwa mtoaji na kwa mpokeji pia.

Katika hatua nyingine ameisisitiza jamii  kutafuta elimu popote walipo wa kiume na wakike kwa jitihada zozote kwani hata katika vitabu vya dini vimeelezea kuitafuta elimu ya dunia na akhera.

Kwa upande wa mashekhe wa misikiti iliyonufaika na sadaka ya iftar  waliishukru taasisi ya Ramadhan Charity kwa kila mwaka kwa kuwapitia Iftar katika kipindi Cha Ramadhani.

"Sisi hatuna chakulipa ila mwenyezi Mungu ndio atawalipa tutazidi kuaombea dua kwa mwenyezi Mungu awajalie neema na awarejeshe tena na tena,ila tunaomba kama inawezekana na misikiti mwingine au vituo vingine kama hajaingizwa kwenye program hii basi vingizwe kupata sadaka hiyo," walisema mashekhe hao.

Taasisi ya Ramadhani Charity Program 2025 imetoa msaada wa mchele, Sukari, tende, unga, Luku kwa ajili ya umeme pamoja na pesa za mboga. Taasisi hii inafanya harakati za kutoa misaada hii kila mwaka na mwaka huu tayari imetoa misaada kwa mikoa mitano na inaendelea kutoa hadi mwisho wa mwezi mtukufu.







 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad