VETA YAADHIMISHA MIAKA 30 NA MAFANIKIO LUKUKI YA UFUNDI STADI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Wednesday, March 5, 2025

VETA YAADHIMISHA MIAKA 30 NA MAFANIKIO LUKUKI YA UFUNDI STADI

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda (katikati) akizungumza na vyombo vya habari katika Ofisi ndogo za Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Magogoni Jijini Dar es Salaamkuhusu Maadhimisho ya miaka 30 ya VETA.

...........................................

Na Mwandishi Wetu, Da es Salaam

WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema miaka 30 ya Mamlka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi(VETA) ni siku ya kusherehekea mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa Serikali katika kuboresha elimu ya Ufundi Stadi nchini.

Hayo yamebainishwa leo Machi 5,2025 na Profesa Mkenda wakati akizungumza na vyombo vya habari katika Ofisi ndogo za Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Magogoni Jijini Dar es Salaam.

Waziri Prof.Mkenda amesema kwamba maadhimisho ya VETA ni sehemu mojawapo yakujikumbusha kwamba bado kuna umuhimu na safari ndefu yakutambua ujuzi wa mafundi walioko mtaani unakuwa na ushindani na kuweza kuongeza kipato katika pato la Taifa.

Aidha, amesema maadhimisho hayo yanakuja naaelekezo ya kujenga mahusiano kati ya VETA na viwanda,ambapo VETA itatoa fursa kwa wanafunzi kwenda viwandani kujifunza kwa vitendo ili kukidhi vigezo katika soko la ndani na kuuza nje ya nchi.

"VETA itajenga mfumo wa wazi na ushindani ili kutambua vijana mafundi wa viwandani ili kutoa fursa kwa vijanq wa VETA kujifunza kutoka kwa mafundi mahiri walioko nchini",amesema Prof.Mkenda

Sanjari na hayo pia amesema maadhimisho haya yanaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya Mfumo wa Kitaifa wa kusimamia mafunzo ya ufundi stadi na miaka 30 ya VETA tangua kuanzishwa kwake mwaka 1995 pia wakati Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameagiza kukamilisha ujenzi wa vyuo vya VETA vya hadhi ya kimkoa katika mikoa yote ambayo haina vyuo,na Hadi sasa chuo cha VETA cha Songwe kimekamilika na ujenzi wa vyuo 64 unaendelea katika Wilaya ambazo hazikuwa na Vyuo vya VETA.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzani Kassim Majaliwa na yatafanyika kuanzia Machi 18 hadi 21,2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad