Wanawake wa Kanisa la Moravian Mkoa wa Singida, wakiwa na vitu mbalimbali kabla ya kutoa kwa msaada kwa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani.
.........................................
Na Dotto Mwaibale, Singida
Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Wanawake wa Kanisa
la Moravian Mkoa wa Singida, wamefanya ziara maalum ya kiinjilisti ya kwenda kuwatembelea
na kuwafariji wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.
Ziara hiyo iliyobeba matendo ya huruma imefanyiika ikiwa na
lengo la kuwafariji, na kuwapa misaada
mbalimbali kama biblia inavyoelekeza kuwajali wenzetu waliokwenye changamoto
mbalimbali zikiwemo na magonjwa.
Wanawake hao wakiongozwa na Mama Mchungaji Daniel Kikoma wamekabidhi
vifaa vitu vya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sukari, Sabuni, dawa za meno
na vinginevyo.
Baada ya kukabidhi vitu hivyo Mama Mchungaji Daniel Kikoma
aliongoza maombi maalumu ya kuwaombea wagonjwa katika hospitali hiyo ili kupata
uponyaji wa Mungu akishirikiana na Mama Mchungaji Yona Ezekiel.
Aidha baada ya kutoka hospitalini hapo walikwenda Kanisa la Moravian Sabasaba ambapo walienda ibada na kazi nyingine ikiwa ni maadhimisho ya siku yao hiyo.
Kilele cha siku ya wanawake Duniani kitaifa kimefanyika leo Jijini
Arusha, ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Wanawake hao wakiwa katika picha ya pamoja.










No comments:
Post a Comment