KATIBU MKUU MTENDAJI (TAHLISO) AWASISITIZA WANAFUNZI KUIMARISHA AMANI, UPENDO NA MSHIKAMANO - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, 17 April 2025

KATIBU MKUU MTENDAJI (TAHLISO) AWASISITIZA WANAFUNZI KUIMARISHA AMANI, UPENDO NA MSHIKAMANO

 

Katibu Mkuu Mtendaji wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Ndg. Godfrey Gilagu, ametoa wito kwa wanafunzi kote nchini kuendelea kuimarisha amani, upendo na mshikamano, akisisitiza kuwa hayo ndiyo nguzo muhimu za mafanikio na msingi wa maelewano bora miongoni mwa Watanzania kama taifa moja.

Ndg. Gilagu ameyasema hayo tarehe 17 Aprili, 2025, wakati wa ziara yake ya kikazi aliyo Muwakilisha Mh.Rais wa (TAHLISO) Ndg. Geofrey Kiliba.

katika Mkoa wa Tabora, katika Chuo Kikuu cha Archbishop Mihayo University College of Tabora.(Amucta).

Ziara hiyo ilikuwa na lengo la 1.Kujitambulisha na kuwafikia Wanafunzi na Mkoani tabora lakini

2.Kusikiliza, Kuchukuwa na kutatua changamoto za Wanafunzi.

3.Kuhimiza wanafunzi kudumisha Amani nchi.

4.Kueleza miradi na Maendeleo kupitia Sekta ya Elimu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad