Mwanasheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), Baraka Chipamba akizungumza na wanafunzi wa Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA), Kampasi ya Temeke jijini Dar es Salaam ambavyo vipo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati akifundisha kuhusu sheria mbalimbali Aprili 28, 2025.
.......................................
Na Mwandishi
Wetu, Dar es Salaam
UFANISI wa
Sheria mbalimbali utaendelea kupata mafanikio iwapo vitendo vya uhalifu
vitakapo ripotiwa kwenye mamlaka husika na hatua kuchukuliwa.
Hayo
yameelezwa Aprili 28, 2025 na Mwanasheria wa Tume ya
Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), Baraka Chipamba wakati akizungumza na
wanafunzi wa Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA), Kampasi ya Temeke jijini Dar
es Salaam ambavyo vipo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Mwanasheria huyo aliyasema hayo wakati akitoa elimu kwa
wanafunzi hao inayohusu makossa ya kimtandao ambayo yanafanywa kwa kutumia
vifaa vya kieletroniki kama vile kompyuta, simu janja, vishikwambi na
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
“ Ufanisi wa sheria zetu utaendelea kupata mafanikio iwapo vitendo vya uhalifu vitaripotiwa kwenye mamlaka husika na kutolewa adhabu kwa watuhumiwa na si vinginevyo,” alisema Chipamba.
Chipamba alitaja baadhi ya makosa ya kimtandao kuwa ni kutuma picha au video za ngono kwa watoto na kuzisambaza, kuwashawishi watoto kuingilia mawasiliano ya kingono kupitia mitandao.
Alisema katika jitihada za kuimarisha ulinzi
wa watoto dhidi ya makosa ya mtandao, Sheria ya Mtoto sura Na. 13, 2009 nchini Tanzania imepitia marekebisho muhimu
ambayo yamezingatia athari za matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika masuala ya ulinzi wa
mtoto kama vile kumlinda mtoto
dhidi ya ukatili mtandaoni, kutuma lugha ya matusi,
kejeli, au ya kuudhi kupitia mitandao, watoto wasidharauliwe, kusambaziwa
ujumbe wa matusi au kudhalilishwa kupitia mitandao ya kijamii.
Chipamba alisema adhabu ya
makossa ya kimtandao ni faini kuanzia Sh. Milioni 3 hadi Milioni 20 au kifungo
cha miaka 7. Ambapo pia alihimiza mtumizi bora ya mitandao ya kijamii.
Aidha katika hatua nyingine, Chipamba alihimiza jamii kujenga tabia ya kuandika wosia kwani unasaidia kupunguza kama
siyo kumaliza kabisa changamoto ya kugombea mali zilizoachwa na marehemu.
“Tujenge dhna ya kuandika
wosia utatusaidia na kuondoa kabisa madhira ya kugombea mali ambazozitaachwa na
marehemu,” alisema Chimpamba.
Kwa
upande wake Mwanasheria Vicky Mbunde kutoka Tume hiyo, akitoa elimu kuhusu
sheria ya ustawi wa wanyama alisema Serikali inawataka wananchi
kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa haki za wanyama ikiwa ni pamoja na kuwapa
stahiki zao.
Alisema sheria na kanuni mbalimbali
zinazolinda haki za wanyama wanaofugwa nchini zinapaswa kulindwa kwani mnyama
ana haki ya kutunzwa vizuri ikiwa ni pamoja na kupewa chakula kizuri, banda ambalo litamkinga dhidi
ya mvua na jua na liwe zuri lenye mwanga wa kutosha.
“ Wanyama wana haki ya kisheria
ya kutibiwa kama anavyotibiwa binadamu hivyo akiwa na changamoto yoyote ya
kiafya mfugaji ana wajibu wa kumpeleka kwa daktari wa mifugo ili aweze kupatiwa
matibabu na kufuata maelekezo yote yatakayotolewa na mtaalam huyo wakati wote
wa matibabu yake,” alisema Mbunde.
Mbunde alisema vitendo vya kumpiga mnyama na
kumnyima stahiki zake ni kosa kisheria na kuwa vinakinzana na sheria ya ulinzi na ustawi wa wanyama namba 19 ya mwaka 2008.
Meneja wa Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA), Kampasi ya Temeke,
Benadeta Kessy akizungumzia elimu walioipata aliishukuru Tume ya
Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) kwa hatua hiyo ya kutoa mafunzo hayo kwa
makundi mbalimbali ambapo aliomba elimu hiyo waipeleke kwenye kampasi zingine
za LITA
Mwanasheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), Vicky Mbunde akizungumza na wanafunzi wa Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA), Kampasi ya Temeke jijini Dar es Salaam kuhusu sheria ya ulinzi na ustawi wa wanyama.
Meneja wa Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA), Kampasi ya Temeke, Benadeta Kessy, akiishukuru Tume hiyo kwa kuwapelekea elimu hiyo.
Mkufunzi Rajab Msami akizungumzia mafunzo hayo ambapo ameahidi kuwa watakuwa mabalozi kwa wengine.
Mwanasheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), Vicky Mbunde, akitoa mafunzo kwa watumishi wa wa Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA), Kampasi ya Temeke.
Wanachuo wa kampasi hiyo wakipata elimu hiyo.
Elimu ikiendelea kutolewa.
Wanachuo hicho wakipata elimu hiyo.
Tswira ya mafunzo hayo.
Mwanafunzi Elizabeth Simon akiuliza swali.
Mwanafunzi Mussa Kilimu akiuliza swali.
Mwanafunzi Melkichezedeky Nabao akiuliza swali.
Mwanafunzi John Kichele akiuliza swali.
Wanafunzi wakipata elimu hiyo.
Wtumishi wa wakala ya Mafunzo ya Mifugo Kampasi ya Temeke, wakipatiwa elimu ya namna ya kuandika Wosia na Ufunguaji wa Mirathi.
Mafunzo kwa watumishi wa kampasi hiyo yakiendelea.
Mtumishi wa Kampasi hiyo Abdallah Mbwana akiuliza maswali mbalimbali.
Mtumishi wa Kampasi hiyo, Nuru Mhagama akitoa neni la shukurani kwa Tume hiyo kwa kuwapelekea mafunzo hayo.
Watumishi wa Kampasi hyo wakiwa katika picha ya pamoja na Wansheria kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria (LRCT), baada ya kuwapatia elimu hiyo.







No comments:
Post a Comment