WADAU WAOMBWA KUDHAMINI TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI MKUU - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Wednesday, 2 April 2025

WADAU WAOMBWA KUDHAMINI TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI MKUU

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion , Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu maandalizi ya tamasha la kuombea uchaguzi mkuu Aprili 2, 2025 jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Barazaa  Makanisa ya Kipenteksote Mkoa  wa Dar es salaam, Mchungaji Emmanuel Mwasota.

....................................................

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

 WADAU mbalimbali na Watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi  kudhamini Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu litakalofanyika  katika mikoa 26 nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari April 2, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion , Alex Msama amesema tamasha hilo halitakuwa na kingilo ili kila mtanzania aweze kushiriki kwenye kuliombea taifa huku maandilizi yakiwa yanaendele vizuri.

 Msama ameongeza kuwa  tamasha hilo litaanzia Mkoa wa Dar es salaam na  kufuatia mikoa mingne na kueleza kuwa litawahusisha Wachungaji na Maaskofu ambao wataongoza maombi maalumu ya kuombea amani nchi kulekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba mwaka huu.

Aidha amesema waimbaji mbalimbali maarufu kutoka nje na ndani ya nchi watakuwepo kwenye tamasha hilo kutoa burudani.

" Dar es Salaam ndipo litakapoanzia tamasha letu hivyo hivi karibuni tutatangaza tarehe na eneo   litakapofanyika," alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Barazaa  Makanisa ya Kipenteksote Mkoa  wa Dar es salaam, Mch  Emmanuel Mwasota amesema  tamasha hilo lipo kwajili ya Maombi ya Kuombea uchaguzi Mkuu kwa kuungana kwa pamoja kwa waumi wote wa madhehebu yote kuiombea nchi yetu, viongozi , wabunge, madiwani na Rais ili uchaguzi uweze kufanyika kwa amani.

"Sisi tumesema ya kwamba tutashikama kwa pamoja na taarifa hizi zinaenda kila mahali kwa  makanisa, wachungaji, maskofu na waubiri wa aina mbalimbali tutakuwa pamoja kuhakikisha tunaombea nchi yetu ipite salama kwenye uchaguzi utakaofanyika mwaka huu," alisema.

Ameongeza kuwa uchaguzi unaweza kusabisha nchi kupasuka kama raia  wake wasipokuwa wazalendo ndio maana tunahitaji kufanya Tamasha hilo maalumu la kuombea nchi na viongozi wetu lengo likiwa nchi yetu iendelee kuwa na amani na utulivu na tuweze kuvuka salama kipindi cha uchaguzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad