WAZIRI MKUU AONGOZA HARAMBEE YA KUFANIKISHA MEI MOSI 2025 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, April 6, 2025

WAZIRI MKUU AONGOZA HARAMBEE YA KUFANIKISHA MEI MOSI 2025

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi 500,000 kutoka kwa Sheikh wa mkoa wa Singida, Sheikh Issa Nassoro Issa katika  harambee ya kuchangisha fedha za kufanikisha  Maadhimisho ya Mei Mosi  2025 kitaifa, Aprili 5, 2025. Zaidi ya shilingi bilioni 1.6 zilichangwa .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  katika harambee ya kuchangisha fedha za kufanikisha Maadhimisho ya Mei Mosi  2025 kitaifa kwenye ukumbi wa hoteli ya Royal Village jijini Dodoma, Aprili 5, 2025. Zaidi ya shilingi bilioni 1.6 zilichangwa kwa ajili ya maadhimisho hayo yatakayofanyika mkoani Singida 01.05.2025
Baadhi ya washiriki wa harambee ya kuchangisha fedha za kufanikisha Maadhimisho ya Mei Mosi  2025 kitaifa wakimsikiliza mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza katika harambee hiyo, Aprili 5, 2025. Zaidi ya shilingi bilioni 1.6 zilichangwa kwa ajili ya maadhimisho hayo yatakayofanyika mkoani Singida 01.05.2025.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiingia kwenye ukumbi wa hoteli ya Royal Village jijini Dodoma, kuongoza harambee ya kuchangisha fedha za kufanikisha  Maadhimisho ya Mei Mosi  2025 kitaifa, Aprili 5, 2025. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego. Zaidi ya shilingi bilioni 1.6 zilichangwa kwa ajili ya maadhimisho hayo yatakayofanyika mkoani Singida 01.05.2025 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na rais wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania  (TUCTA), Tumaini Nyamuhokya alipowasili kwenye ukumbi wa hoteli ya Royal Village jijini Dodoma kuongoza harambee ya kuchangisha fedha za kufanikisha  Maadhimisho ya Mei Mosi  2025 kitaifa, Aprili 5, 2025. Zaidi ya shilingi bilioni 1.6 zilichangwa kwa ajili ya maadhimisho hayo yatakayofanyika mkoani Singida 01.05.2025 
................................................

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yana lengo la kuhamasisha utoaji wa haki za wafanyakazi, kuboresha masharti ya kazi na ustawi wa wafanyakazi kwa ujumla.

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo jana usiku, Aprili 5, 2025 katika hafla ya chakula cha jioni kwa ajili ya kuchangisha fedha za kugharamia maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Singida. Hafla hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa Royal Village jijini Dodoma.

Amesema dhumuni jingine la maadhimisho hayo ni kutambua na kuenzi michango ya wafanyakazi katika maendeleo ya jamii na uchumi, Mei Mosi ni fursa ya kuonesha mshikamano kati ya wafanyakazi na kuhimiza usawa na haki katika maeneo ya kazi duniani kote.

Waziri Mkuu amesema mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika hafla hiyo jumla ya shilingi bilioni 1.62 zilikusanywa  zikiwa  ni ahadi na fedha taslimu, lengo lilikuwa ni kukusanya sh milioni 832.8.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete, rais wa TUCTA, Tumaini Nyamuhokya, Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Martha Mlata.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad