MAAFISA WATENDAJI WAKUU (MA CEO) WATARAJIWA WAKUTANA SINGIDA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, 11 May 2025

MAAFISA WATENDAJI WAKUU (MA CEO) WATARAJIWA WAKUTANA SINGIDA

       Maafisa Watendaji Wakuu wa Makampuni (MA CEO) watarajiwa wakiwa katika kikao kazi kwa ajili a kujadili mikakati yao kupitia jukwaa lao la Young CEO.

............................................... 

Na Mwandishi Wetu, Singida

MAAFISA Watendaji Wakuu wa Makampuni (MA CEO) watarajiwa wamekutanao mkoani Singida katika kikao kazi kwa ajili a kujadili mikakati yao kupitia jukwaa lao la Young CEO.

Mwenekiti wa jukwaa hilo Mkoa wa Singida, Husseni Mseule akizungumza na waandishi wa habari Manispaa a Singida Mei 9, 2025 alisema Young CEO ni platform inayo waunganisha vijana wenye ndoto za kuwa maafisa watendaji wakuu ili kupaza sauti na kufikia ndoto zao.

“ Young CEO ni muunganiko wa wakurungenzi vijana wanao wasaidia vijana wenzao wenye ndoto  za kuja kuwa wakurugenzi na kufikia malengo yao na dhima ao kubwa ikiwa ni kuwaleta pamoja kupitia fani zao mbalimbali kama ujasiriamali, wasanii, wafanya biashara,wanamziki, Baba na Mama LISHE,saluni na wakulima huku maafisa watendaji wakuu hao wakiwa ni waajiri wao kutokana na kuwa na uwezo wa kuajiri,” alisema Mseule.

Mseule alisema mbeba maono na muanzilishi wa jukwaa hilo ni Jeiely Petro (Maarufu kama Sky ) ambaye alithubutu na kuanzisha jukwaa hilo ambalo ni la muhimu kwa vijana.

Mseule alisema moja ya lengo la kikao hicho ilikuwa ni kubadilisha jukwaa hilo na kuifanya kuwa taasisi ili kufungua fursa mbalimbali na wamefikia hatua hiyo baada ya kupata ushauri kutoka kwa walezi na watu wengine ambao waliwaeleza kuliacha jukwaa hilo au kuendelea kuwa kama kikundi ni kubana fursa na kushindwa kupanua wigo mpana na kuwafikia vijana wengi nchini.

Alisema maazimio ya wajumbe wa kikao hicho ni kusajili taasisi itakayojulikana kwa jina la Global change Maker Generation (GMG) itakayosimamiwa na Singida Young CEO.

Kikao hicho kilichofanyika KBH Hoteli kiliudhuriwa na wajumbe nane, Mwenyekiti wa jukwaa hilo,  Hussein Mseule,Katibu Moze Muna, Mweka Hazina, Evaline Mboya, Happyness Juma, Mariam Mtaturu, Mwanzilishi wa jukwaa hilo, Sky, Suphian Juma, Frank Musibha na walezi wa jukwaa hilo.

Kikao kikiendelea.
Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao hicho.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad