Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi,
wadau na wanachana wa Jukwaa hiloNa Godwin Myovela, Morogoro
MKUU
wa Mkoa Adam Kighoma Malima amewataka wana-ushirika wote
mkoani hapa kutambua kuwa ushirika sio msaada, bali ni nguvu ya pamoja
ya kujisaidia – na njia bora ya kuondoa umaskini kwa heshima na mshikamano.
Alisema
mafanikio ya vyama hivi hayawezi kupatikana bila uwajibikaji wa
kweli ambao ndio msingi wa uaminifu. Bila uaminifu, hakuna ushirikiano wa
kweli. Na bila ushirikiano, hakuna maendeleo.
Malima
aliyasema hayo jana wakati akizindua Jukwaa la 5 la Maendeleo ya Ushirika mkoa
wa Morogoro, lenye kauli mbiu isemayo ‘Ushirika hujenga ulimwengu ulio bora.’
“Ushirika
ni nguzo ya jamii jumuishi na chombo thabiti cha kujenga ulimwengu ulio bora
kuanzia vijijini, sote tunaweza kuondoa kabisa umasikini kupitia ushirika
sababu kila kitu kimerahisishwa, ikiwemo upatikanaji wa huduma za
kifedha, masoko ya bidhaa, pembejeo za kilimo kwa bei nafuu,” alisema
Akihamasisha
takribani vyama 226 vinavyounda jukwaa hilo mkoani hapa, mathalani, namna kilimo
pekee kinavyoweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi, alieleza namna ya kufunga
mkanda na kukikabili kama biashara kubwa, kwa kutumia mbegu bora, zana za
kisasa, umwagiliaji wa uhakika, na kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuyauza.
Alisema
kilimo huajiri watu wengi, hasa vijijini, huongeza kipato cha wakulima na
kuchochea matumizi, huzalisha chakula cha ndani na kupunguza utegemezi wa
uagizaji, pia mazao yake ni malighafi kwa viwanda, huongeza mauzo ya bidhaa
ndani na nje ya nchi, zaidi mahitaji ya kilimo huchochea maendeleo ya barabara,
teknolojia, fedha, masoko, na maghala.
Pia
kwa wafugaji na wachakataji wa mazao ya mifugo, alihimiza kuacha tabia za
uchakachuaji hasa maziwa ambayo baadhi ya wafugaji hudiriki kuweka sukari, maji
na ugoro ili kuongeza uzito, jambo ambalo siyo tu ni udanganyifu, bali ni
hatari kubwa kwa afya za walaji.
“Leo
nimeshtuka kusikia kiwango cha utoaji maziwa kwa ngombe mmoja hapa ni chini ya
lita 3! na pia kuna viashiria vya udanganyifu kwenye biashara hii. Natoa
maelekezo kwa Mrajisi Msaidizi na maafisa ushirika wa maeneo husika kuunda mara
moja Amcos 8 za wafugaji 4 kutoka Mvomero na 4 Kilosa ili tuanze nao kwenye
mafunzo kama darasa la mfano kwa wengine, tuone tatizo liko wapi,” alisema
Malima na kuongeza;
“Dhana
ya mafunzo haya ni kuongeza viwango na ubora wa maziwa na mazao mengine ya
mifugo kwa afya, uchumi, soko, usalama, na maendeleo ya sekta ya mifugo kwa
ujumla.”
Zaidi
alisisitiza umuhimu wa wanaushirika kufanya tathmini za kila mwaka ili kubaini
mafanikio na changamoto, katika muktadha wa maboresho kwenye huduma na utendaji
wa chama, uwajibikaji wa viongozi, kulinda maslahi, sanjari na kuweka msingi wa
maendeleo endelevu.
“Ushirika
una nidhamu yake, wale wanaoingia huku kwa lengo la kutupiga tuwakatae, na adui
yetu mkubwa hapa ni ubadhirifu…tusikubali mana unapunguza mapato ya
wanaushirika, unavunja imani ya wanachama, unadhoofisha huduma, na hatimaye
unaweza kuua chama kabisa,” alisema RC Malima huku akionya
kwamba ubadhirifu hautavumiliwa, wala kuachwa kuendelea ndani ya vyama vya
ushirika bila kuchukuliwa hatua kali.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi,
wadau na wanachana wa Jukwaa hiloMwenyekiti
wa Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoa wa Morogoro Mwalimu Iddi Bilali
akizungumza,
Wanachama na wadau wa Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Morogoro wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano wa 5 wa Jukwaa hilo.










No comments:
Post a Comment