SAFARI YA MWANASIASA MKONGWE NA NDOTO YA KUWA RAIS - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Wednesday, 21 May 2025

SAFARI YA MWANASIASA MKONGWE NA NDOTO YA KUWA RAIS

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Makini Coaster Jimmy Kibonde akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama hicho.

......................................... 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

CHAMA Cha Makini kimewatangaza wagombea wake watakao simama kupeperusha Bendera ya Chama hicho kwa ngazi za Urais Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Mkutano huo wa kuchagua viongozi ulifanyika Mei 17,2025 Jijini Dar es Salaam ambapo Coaster Jimmy Kibonde aliteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho na mgombea mwenza Azah Ally Suleiman huku

 Ameir Hassan Ameir mgombea Urais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mara baada ya kutangazwa kuwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho Kibonde amesema  safari ya kuwa mwanasiasa ilianza miaka mingi iliyopita ambapo nilianza nikiwa mwanachama wa kawaida tu katika chama changu,niliendelea mpaka kushika nyadhifa mbalimbali katika chama na mpaka napitishwa kwenye nafasi hii ya kwenda kupeperusha Bendera ya chama  nilikuwa na na nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa.

 Kwa hatua hii niliyofikia naamini ya kwamba ndoto zangu zitatiamia katika maisha yangu.

Ninachukua fursa hii kwa wanachama  na wajumbe wote wa mkutano mkuu kwa kuniamini kunipa nafasi hii ndani ya chama nami ninaahidi kufanya kazi zangu kwa weledi na ufa is kupitia sera za chama.

Kibonde amesema dira ya chama ni kuhimiza,kushawishi na kuwawezesha watanzania kubobea katika Elimu hasa elimu ya Sayansi na Teknolojia toka ncho yoyote Dunia kwa gharama yoyote ile kwa ajili ya kukuza uchumi na maendeleo  ya kijamii ya Tanzania.

Aidha,ameeleza kuwa tunawaomba watanzania kukiunga mkono chama kwa  sera tutakazo zitoa kwenye majukwaa ,sera  zinazozingatia Sheria na kanuni "kauli mbiu ya chama"Hatulali usingizi,tukilala usingizi nchi itauzwa.

Pia amesema kuwa atajitahidi kuleta mapindizu makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,Afya,kilimo pamoja na ajira.

Amesisistiza kwamba katika vipaumbele vyangu katika sekta ya elimu nitatoa elimu bure kuanzia elimu ya awali Hadi chuo kikuu, Huduma ya Afya kwa akina mama wajawazito ni Bure kliniki hadi kujifungua pamoja na kuanzisha bima ya afya ambayo nitaipa jina la MAKINI na hii itakuwa kwa Kila mtazania kwa gharama nafuu wazee pamoja na watoto

Sanjari na hayo aliendelea kwa kusema kwamba kwa upande qa kilimo nitatoaa hekali Tano kwa kila kijana wa  kitanzania aliefikisha miaka 21 na kuhakikisha pembejeo zinapatikana kwa wakati pamoja na kupeleka zana za kilimo kama matrekta Kila Kijiji a vitongoji ili wakulima waondokane na kilimo chakutumia jembe la mkono.

Aliendelea kwa kusema katika sekta ya viwanda nitafanya mabadiliko yatakayoendana na teknolojia ya sasa pamoja na nitajitahidi kuongeza ajira milioni mbili kwa mwaka ili vijana  wengi wapate ajira.

Sambamba na yote nitajitahidi mabadiliko yote nitakayoweka yawanufaishe wananchi wote kwa kuhakikisha fursa za maendeleo zinapatikana kwa Kila Mtanzania.

Katika hatua nyingine nitahakikisha kuleta maendeleo ya kweli na kuwapa  haki wananchi  wote bila ubaguzi.

"Chama Cha Makini kina viongozi waadilifu wenye dhamira yakuleta maabadiliko makubwa katika utawala wa nchi.Endapo nitakuwa rais naahidi kuimarisha mshikamano wa kitaifa ili Tanzania iwe kwenye maendeleo yatakayonufaisha kila mwananchi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad