WAZIRI MASAUNI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KUTEMBELEA KAMPUNI YA UKUSANYAJI NA UTENGENEZAJI TAKA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Wednesday, 14 May 2025

WAZIRI MASAUNI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KUTEMBELEA KAMPUNI YA UKUSANYAJI NA UTENGENEZAJI TAKA

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  (Muungano na Mazingira) Mhe.Mha.Hamad Masauni akiwa na wataalamu wa mazingira walipotembelea kampuni ya Hafslund Celsion inayojishughulisha  na ukusanyaji na  utengenishaji wa Taka katika Mainispaa ya  Oslo nchini Norway. 

........................................

Na Mwandishi Wetu, Norway

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  (Muungano na Mazingira) Mhe.Mha.Hamad M.Y Masauni ameongoza ujumbe wa Tanzania  kutembelea kampuni ya Hafslund Celsion, kampuni inayojishughulisha  na ukusanyaji na  utengenishaji wa Taka katika Mainispaa ya  Oslo nchini Norway. 

Katika Ziara Hiyo Mhe Masauni aliambatana  na  Bi.Tone Tinnes, Balozi wa Norway nchini Tanzania pamoja na Maafisa kutoka Ubalozi wa Norway nchini Tanzania. 

Kupitia ziara hiyo Ujumbe wa Tanzania ulipata fursa ya kujionea jinsi Kampuni hiyo inavyotumia mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa Taka, Jinsi  invyotenganisha Taka na kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwapo Umme.

Jiji la Oslo lina wakazi wapatao 725,000 ambapo kulingana na taarifa za mwaka 2023 kila mkazi huzalisha takribani kilo 157 za taka kwa Mwaka. 

Kampuni ya Hafslund ilianza kazi ya utenganishaji taka mwaka 2012.Ili kuhamasisha utenganishaji wa Taka Kampuni hiyo imekuwa ikitoa bure mifuko ya aina tatu ya kuhifadhia Taka, ambapo Mfuko wa Kijani umekuwa ukitumika kwa ajili ya taka za aina ya vyakula, Mfuko wa Zambarau taka za plastick na taka zinginezo huhifadhiwa katika mfuko wa Rangi Nyeupe. 

Akielezea jinsi kampuni hiyo inavyofanya kazi Mshauri wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Mads. A.Danielsen amesema kampuni hiyo ina matawi matano ambayo yanajihusisha na upokeaji wa Taka zitokanazo na mimea, vigae,vyuma chakavu, fenisha zilizovunjika na magodoro taka hizi hujulikana kama Taka zenye ujazo mwingi ( Bulky Waste). 

Taka zingine ni taka hatarishi,taka zitokanazo na vifaa vya Umeme na taka zinazoweza kurejelezwa kwa Matumizi Mengine.

Ili kuhakikisha kuwa wananchi wa Jiji la Oslo wanatenganisha taka bila shurti, Bw. Danielsen amemweleza Mhe. Masauni na ujumbe wake kuwa, wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kuelimisha Umma ikiwa ni pamoja na sinema, redio,magazeti, broshua, watu maarufu, mabango, matangazo kwenye vyombo vya usafiri, mitandao ya kijamii, muongozo wa kutenganisha taka, maonesho na shughuli mbalimbali za uhamasihaji.

Utenganishaji huo wa Taka umeiwezesha Kampuni ya Hafslund kuanzisha baadhi ya biashara kama  uzalishaji maji yanayotokana na Mvuke unazalishwa baada ya kuunguza  Taka, Biashara ya Umeme, Biashara ya  KaboniUzalishaji wa Mbolea na uuzaji wa Vitu na vifaa vilivyotupwa ambavyo vinaweza kutumiwa na watu wengine. 

Baada ya mkutano huo Ujumbe wa Tanzania ulipata fursa ya kutembelea kiwanda hicho na kujionea hatua mbalimbali za utenganishaji taka. 

Kama nchi zingine duniani Tanzania nayo inazalisha taka hivyo utenganishaji wa  taka hutoa fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzalisha bidhaa zingine zenye manufaa na kuzalisha ajira.

Muonekano wa kiwanda cha kuchakacha takataka kilichopo Norway 
Maelezo kuhusu kiwanda hicho akitolewa.
Kikao kikifanyika

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad