Meneja wa Barrick nchini, Dk.Melkiory Ngido akimkabidhi mfano wa hundi shilingi billioni Tsh 93.6 kwa mheshimiwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye hafla ya siku ya gawio iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam, wengine pichani ni Waziri wa Nchini Ofisi ya Rais (Uwekezaji ) Profesa Kitilla Mkumbo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Twiga Andrew Mwangakala.
Rais wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania , Dkt Samia Suluhu Hassan akikabidhi tuzo kwa
mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Kampuni ya Twiga Minerals , Andrew
Mwangakala na Meneja wa Barrick
nchini,Dk.Melkiory Ngido na wa kwanza kushoto ni Waziri wa Nchini Ofisi
ya Rais (Uwekezaj ) Profesa Kitilla Mkumbo.
---------------------------------------------
Na Damas Mwakangale
KATIKA
kudhihirisha kuwa ubia kati ya kampuni ya Barrick Gold Corporation na Serikali
ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals Corporation unaendelea kunufaisha
pande zote mbili, Migodi ya Barrick
nchini imetoa gawio la shilingi bilioni 93.6 kwa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na kutunukiwa tuzo ya nafasi ya Kwanza katika makundi
ambayo Serikali ina hisa chache kwa mwaka huu.
Hundi ya
gawio hilo (Dummy cheque) imekabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan na Meneja wa Barrick nchini, Dkt Melkiory Ngido, katika hafla ya Serikali
kupokea Gawio na michango kutoka kwa
taasisi na mashirika ya umma (Gawio Day 2025)
iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam
Mwaka wa fedha
wa2022/23 kampuni ya Barrick nchini pia ilishika nafasi ya kwanza kutoa gawio
kwa Serikali ya kiasi cha shilingi bilioni 84 ambapo mwaka jana ilishika nafasi
ya pili kwa kutoa gawio ya kiasi cha shilingi bilioni bilioni 53,482,072,393.
Migodi
iliyopo chini ya kampuni ya Barrick na Twiga Minerals nchini ni North Mara na
Bulyanhulu na Buzwagi ambao upo katika mchakato wa kufungwa.
Akiongea juu
ya mafanikio haya, Meneja wa Barrick
nchini,Dk.Melkiory Ngido alisema Barrick na Twiga Minerals mbali na
kutoa gawio nono kwa Serikali pia imekuwa ikichangia pato la Serikali kupitia
malipo ya tozo mbalimbali katika maeneo
yenye shughuli za migodi yake sambamba na kuchangia kukuza uchumi wa Taifa
kupitia kodi, ushuru, magawio, mishahara na malipo kwa wazabuni wa ndani .
Aliongeza
mbali na kutoa gawio la kuchangia pato la Serikali,uwekezaji wa kampuni ya
Barrick nchini unaendelea kuboresha maisha ya wananchi kupitia miradi
inayotekelezwa kwenye maeneo yanayozunguka migodi yake kwa fedha za uwajibikaji
kwa jamii (CSR) zinazotolewa na migodi inayoimiliki ya North Mara na
Bulyanhulu.
Kwa upande
wake . Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu
akiongea katika hafla hiyo alisema kampuni ya Twiga Minerals imekuwa
ikifanya vizuri kwenye sekta ya uchimbaji wa madini nchini kwa kadri siku
zinavyozidi kusonga mbele.
Mchechu alisema kwamba kwa mwaka huu serikali imepata Tsh 1.28 Trillioni kama gawio , michango na makusanyo mengineo ambazo zinakwenda kuboresha sekta ya elimu , afya , miundombinu na sekta zingine mtambuka kwenye uchumi wa nchini.









No comments:
Post a Comment