MBUNGE DKT. FLORENCE SAMIZI ATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE SEKONDARI YA RUBANGA KIGOMA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, June 26, 2025

MBUNGE DKT. FLORENCE SAMIZI ATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE SEKONDARI YA RUBANGA KIGOMA

Katibu wa Mbunge, Dorice Nsekela (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Rubanga baada ya kuwakabidhi taulo kwa niaba ya Dkt. Florence Samizi Mbunge wa Jimbo la Muhambwe katika hafla iliyofanyika Juni 25, 2025.

....................................

Na Mwandishi Wetu, Kibondo

MBUNGE wa Jimbo la Muhambwe Dkt. Florence Samizi ametoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Rubanga iliyopo Kata ya Rusohoko Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.

Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakipokea msaada huo walisema unakwenda kuwawezesha kuwa katika hali nzuri ya masomo na chachu ya kusoma kwa bidi na kumuahidi mbunge huyo kuwa watafanya vizuri kwenye masomo yao na kufikia ndoto zao za maisha.

“Tunakushukuru sana mbunge wetu kwa msaada huu ambao umetupa mori wa kusoma pia tunaamini utakuja tena na kutufanyia makubwa zaidi ya haya uliotufanyia,” alisema mmoja wa wanafunzi hao.

Mkuu wa Shule hiyo, Gervas Makunda alisema Mbunge Samizi amekuwa kiungo bora kwa kuimarisha miundombinu ya shule hiyo hivyo kila mpenda maendeleo katika wilaya hiyo anapaswa kumuunga mkono kwa jitihada zake hizo.

“Serikali kupitia mbunge wetu huyu walituwezesha kutuletea maji ambayo yanatoa huduma kwa wafanafunzi 670 huku kiasi kikubwa kikitumika kwenye vyoo na hiyo inatokana na kujengwa eneo lenye milima,” alisema Makunda.

Alisema idadi hiyo ya wanafunzi itaongeza na kufikia wanafunzi zaidi ya 800 hali ambayo itakuwa ni changamoto kubwa ya maji ambapo ameiomba Serikali kupitia mbunge huyo waweze kusaidia kuchimbiwa kisima kikubwa cha maji kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa maji ya kutumia kwa kufanya usafi wa vyoo na madarasa.

“Tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na mbunge wetu Dkt. Samizi kwa misaada mbalimbali wanayoitoa kuinifaisha shule yetu kwani wangeweza kuipeleka katika shule nyingine lakini wakaona wailete hapa kwetu Rubanga,” alisema Mwalimu Masanja Malaba.

Wananchi wa kata hiyo wamemuelezea mbunge huyo kuwa yupo mstari mbele kuwapambania kuwapelekea maendeleo katika sekta mbalimbali.

“Wamepita wabunge wengi lakini hawakuwa majembe kama alivyo Florence Samizi tunapaswa kumchagua kwa kura nyingi ili aendelee kutufanyia makubwa zaidi na kama tungemchagua mwingine hizi fursa zote tunazozipata kupitia kwake tungezipata wapi?,” alihoji mmoja wa wakazi wa kata hiyo.

Wanafunzi hao wakionesha furaha zao baada ya kupokea msaada huo kutoka kwa Mpendwa Mbunge wao, Dkt. Florence Samizi..
Wanafunzi wakionesha taulo baada ya kukabidhiwa.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad