ALEX MSAMA BAADA YA JINA LAKE KUKATWA AOMBA KUTOA USHIRIKIANO KWA WALIOTEULIWA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Wednesday, July 30, 2025

ALEX MSAMA BAADA YA JINA LAKE KUKATWA AOMBA KUTOA USHIRIKIANO KWA WALIOTEULIWA

Ndugu Alex Msama akiwa katika moja ya kikao baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Ukonga lililopo Ilala Jijini Dar es Salaam.

.............................................................

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Siku moja tu baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuondoa jina lake miongoni mwa watia nia wa Jimbo la Ubunge Ukonga jijini Dar, aliyetia nia, Alex Msama ametoa neno zito.


Msama ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Msama Promotions & Dira Media ametoa neno kwa kuwataka watia nia wote waliokatwa majina yao nchini kote kutoa ushirikiano kwa wale ambao majina yao yanakwenda kupigiwa Kura za Maoni ngazi ya kata na hatimaye kumpata mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Huyu hapa Alex Msama: "Nilitia nia kuomba kuteuliwa na chama changu kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga. Lakini isivyo bahati jina langu halikurudi.

"Siyo kwamba sifai. Nafaa ila jina langu halikurudi. Kwa wakati huu wamepatikana wengine ambao wamepewa nafasi na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama chetu ili kuendelea na mchakato.

"Sisi sote ni wana CCM. Kwa hiyo wote tuna sifa ila waliopitishwa wanafaa kwa sasa. Nawaomba watia nia wengine wote ambao pia majina yao hayakurudi, tuwape ushirikiano wale ambao majina yao yamerudi. Hiki ni kipindi cha kushikamana badala ya kusambaratika.

"Kwa hiyo niwaombe wale wote waliotia nia kama mimi lakini majina yao hayakurudi, tushikamane kwa nia ya dhati ya kuendelea kukiweka chama chetu katika umoja ili kumsaidia Mwenyekiti wa CCM-Taifa. Mama yetu, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan."

Msama aliendelea kusema kuwa, katika kipindi hiki hategemei kuwepo kwa makundi kwa sababu ya majina yao kutorudi au kukatwa.

Akasema: "Kama watia nia wenzangu walimsikiliza vizuri Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla baada ya kumaliza kusoma majina yaliyorudi, alisema wote ambao majina yao hayakurudi tuwe watulivu bado chama kina mahitaji mengi. Kwa hiyo tutulie na kushikamana."

APONGEZA MAREKEBISHO MADOGO YA KATIBA CCM 

Akizungumzia marebebisho madogo ya katiba ya chama hicho ya kuomba ridhaa kwa wajumbe wa mkutano mkuu kuruhusu kuongeza idadi ya wagombea badala ya watatu alisema ni hatua nzuri na hiyo inaonesha jinsi CCM kilivyo na Ddemokrasia na kueleza kuwa ni chama cha watu na si cha mtu mmoja.

Alisema hatua hiyo imeondoa malalamiko ambayo yangeweza kujitokeza kwa baadhi ya wagombea ambao walikuwa wakiwania nafasi za ubunge, udiwani na baraza la uwakilishi kwa kushindwa kuingia katika nafasi ya tatu ambayo iliwekwa kabla ya kufanya marekebisho hayo.

"Niipongeze kamati kuu chini ya Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa kwa kuwa na maono ya kulitambua jambo hilo ambalo limekuwa na manufaa makubwa kwa wagombea," alisema Msama.


 Ndugu Msama alipokuwa akikabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo la Ukonga,

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad