BETWAY YAINGIA MKATABA WA SH. BILIONI 20 WA MIAKA MITATU NA SIMBA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Tuesday, July 29, 2025

BETWAY YAINGIA MKATABA WA SH. BILIONI 20 WA MIAKA MITATU NA SIMBA




Hafla ya kukabidhiana hundi baina ya Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Betway Tanzania na klabu ya Simba ikifanyika baada ya kuingia mkataba wa udhamini na klabu ya Simba SC wenye thamani ya Shilingi bilioni 20 kwa kipindi cha miaka mitatu.
................................

Na Kelvin Kijo, Dar es Salaam

Kampuni ya michezo ya kubahatisha, Betway Tanzania, imeingia mkataba wa udhamini na klabu ya Simba SC wenye thamani ya shilingi bilioni 20 kwa kipindi cha miaka mitatu, ikiwa ni moja ya mikataba mikubwa zaidi katika historia ya michezo nchini.

Akizungumza katika hafla ya kupokea hundi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally, alisema udhamini huo ni hatua kubwa kuelekea mageuzi ya soka nchini na Afrika kwa ujumla.

“Udhamini huu ni mwanzo wa mapinduzi makubwa kwenye sekta ya michezo hapa Tanzania. Takwimu zinaonyesha Simba ni moja ya klabu bora Tanzania na hata Afrika. Lengo letu ni kuipeleka Simba kuwa klabu bora barani,” alisema Ahmed.

Kwa upande wake, Mkuu wa Udhamini wa Betway, Bw. Jason Shield, alieleza kuwa kampuni hiyo imekuwa ikifuatilia kwa karibu maendeleo ya Simba SC na imejiridhisha kuwa klabu hiyo inastahili uwekezaji huo mkubwa.

“Hatukukurupuka. Tumeichunguza Simba kwa muda mrefu na tunaamini mkataba huu utaongeza thamani kwa pande zote—Simba, Betway, na mashabiki. Ndani ya miaka mitatu, matunda ya uwekezaji huu lazima yaonekane” alisema Bw. Shield.

Naye Meneja Mtendaji wa Betway Tanzania, Bw. Jimmy Masaoe, aliongeza kuwa wameboresha mfumo wao wa huduma kwa wateja ili kuendana na ukuaji wa soko.

“App yetu sasa ina huduma bora zaidi, tumeboresha muonekano na matumizi (‘user experience’), tumepanua huduma za kituo cha wateja (call center), pamoja na kushirikiana zaidi na jamii ambao ndio wadau wetu wakubwa” alisema.

Meneja Mtendaji wa Betway, Mr. Jimmy Masaoe, akizungumza wakati wa kuhitimisha hafla hiyo, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Athuman Jumanne Nyamlani, aliipongeza Simba SC kwa kupata udhamini huo mkubwa.

“Ubora wa klabu zetu na ligi yetu umewavutia wadhamini wa kimataifa kama Betway. Hii ni nafasi ya Simba kuongeza ushindi, kuboresha miundombinu, na kuhakikisha ripoti ya utekelezaji wa mkataba inatolewa kwa uwazi. Hatutaki migogoro ya udhamini,” alisisitiza Bw. Nyamlani.

Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Athuman Jumanne Nyamlani, akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Meneja Mtendaji wa Betway Tanzania, Bw. Jimmy Masaoe, akichangia jambo wakati wa hafla hiyo.
Meneja Mtendaji wa Betway, Mr. Jimmy Masaoe  

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad