Mkuu wa Wilaya ya Kahama Frank Nkinda ambaye alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Momba mkoani Songwe akilia wakati wa tukio la kuagwa kwake lilifanyika Julai 11, 2025 wilayani Momba. Nkinda alietuliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama.
...............................................
Na Mwandishi Wetu, Songwe.
WAKAZI wa Tindingoma Wilaya ya Momba mkoani Songwe katika makundi tofautitofauti (Viongozi wa Chama,Wazee, Wamama, Wajasiriamali, Bodaboda, Watoto) wamejitokeza kwa hiyari kumuaga aliyekua Katibu Tawala (DAS) wa Wilaya ya Momba Mhe. Frank Nkinda ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Wakiwa katika majonzi makubwa yaliyotokana na namna Nkinda alivyoishi nao kwa kipindi cha Miaka Miwili akiwa kama Katibu Tawala. Akiishi falsafa yake ya “Maisha ni watu, maisha ni mahusiano na utu una thamani kuliko Cheo”.
Wana Momba wamemuaga kwa utumishi wake wa upendo na wadhati ndani ya Momba na kumtakia kila lenye kheri katika nafasi yake mpya ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama.
Aidha, Mhe. Nkinda amewashukuru kwa dhati wakazi wa Tindingoma- Momba kwa ushirikiano waliompa kwa kipindi chote cha utumishi wake huku akiwaomba kuendelea kumuombea katika utumishi wake Mpya katika nafasi na Ukuu wa wilaya ya Kahama na akiwaomba kumpa ushirikiano DAS Mpya kama walivyompa ushirikiano alivyokua DAS.
Hali ilivyokuwa wakati wa tukio hilo la kumuaga DC Nkinda.Wananchi wakimpa mkono wa kwaheri kiongozi wao.
Ni mwndo wa uagana kwa kukumbatiana kwa huzuni
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kuagwa.








No comments:
Post a Comment