MkurugenziMkuuwaJKBRS Dk. Riziki Buberwa akionesha aina mbalimbali za dawa za asili zinazozalishwa na kampuni yake kwenye maonesho ya Wiki ya Tiba Asili kitaifa yanayofanyika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma (Agosti 25-31) mwaka huu
..............................................
Na Godwin Myovela, Dodoma
Wananchi wa Dodoma na maeneo jirani wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutembelea banda la taasisi ya JKBRS kwenye maadhimisho ya Wiki ya Tiba Asili yanayofanyika kwenye viwanja vya Chinangali Park, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Mkurugenzi Mkuu wa JKBRS, Dk. Riziki Buberwa alisema taasisi yake imejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, dawa zenye ubora wa kitaifa na kimataifa, pamoja na ushauri wa kitaalamu kutoka kwa madaktari waliobobea.
“Tumeandaa aina za dawa zilizothibitishwa na ambazo pia mpaka sasa zinaendelea kutumika kwenye jumla ya hospitali za rufaa 14 za serikali nchini.
Dawa hizi ni salama, zenye ushahidi wa kisayansi na zimekuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa wenye changamoto mbalimbali za kiafya.
"Tunawakaribisha wananchi wote waje wajionee ubora na ufanisi wake,” alisema Dk. Buberwa.
Alibainisha kuwa baadhi ya dawa ambazo wananchi watazipata kwenye banda la JKBRS ni pamoja na prostax kwa tiba ya tezi dume, tanzax treatment kwa matatizo ya figo, dental formular power kwa matatizo ya meno na kinywa, na allergex kwa aleji mbalimbali.
Dawa nyingine ni s.one kwa matatizo ya macho, filopex kwa matatizo ya vimbe kwenye kizazi na kuzibua mirija, gotex kwa matatizo ya baridi yabisi na nurosicol kwa changamoto za kiharusi (stroke).
Aidha, katika maonesho hayo ambayo yanatarajia kutamatika Agosti 31 mwaka huu, Buberwa alisisitiza kuwa JKBRS pia imeboresha dawa zinazosaidia mifumo ya mwili ikiwemo mfumo wa uzazi, homoni, shinikizo la damu na mfumo wa fahamu.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Tuimarishe Huduma za Tiba Asili zenye Ushahidi wa Kisayansi."
"Sisi JKBRS tumeitikia kwa vitendo kwa kuja na suluhisho la afya zinazokidhi viwango vya kimataifa. Wananchi wasikose kutembelea banda letu – watapata tiba, elimu, na ushauri wa kitaalamu,” aliongeza.
Aliongeza kuwa nje ya maonyesho haya, JKBRS hupatikana jijini Dar es Salaam, katika jengo la Ubungo Plaza, ambapo huduma na dawa hizo zinatolewa kila siku kwa wananchi wote.
Kwa mujibu wa Dk. Buberwa, lengo kubwa la JKBRS ni kuhakikisha tiba asili inakuwa chachu ya afya njema na sehemu ya suluhisho la changamoto zinazowakabili Watanzania wengi.
0 Comments