Na. Sgt. Geofrey Jacka - DODOMA
Mkuu wa
Jeshi la Magereza Nchini CGP. Jeremiah Yoram Katungu, amewataka Maafisa na
Askari wa Jeshi la Magereza, kujiwekea malengo na kufanya tathmini ya utendaji
wao, ili kujua kipi kimefanyika kwa mafanikio na ambacho hakijafanyika ili
kukiwekea mikakati ya utekelezaji.
CGP.
Katungu amesema hayo Septemba 25, 2025 wakati akizungumza na Maafisa na Askari
wa Jeshi la Magereza Makao Makuu, ambapo pia aliwapongeza Watumishi wote nchi
nzima kwa kazi nzuri wanazofanya, na kuhimiza wawe na uthubutu, ubunifu na kutenda
haki katika utendaji wao kwani hakuna jambo lisilo wezekana.
"Kwanza
kabisa niwapongeze Watumishi wote wa Jeshi la Magereza nchi nzima kwa kazi
nzuri zinazo endelea kufanyika, lakini niwatake muwe na tabia ya kujifanyia
tathmini wenyewe ili kujua kama malengo mliyojiwekea yanatimia, na muwe na
uthubutu wa kufanya mambo kwasababu hakuna kinacho shindikana, na uzuri
rasilimali zipo" alisema CGP. Katungu
Aidha,
CGP. Katungu ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Magereza
kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kwa kulipatia vyombo vya usafiri na
kupunguza changamoto iliyo kuwepo, kuwezesha kuimarisha mifumo ya kiusalama kwa
kufunga vifaa vya kisasa vya upekuzi (walk through scanner) katika Magereza
yetu pamoja na matumizi ya TEHAMA katika utendaji wa Jeshi.
Pia
CGP. Katungu amesema, Jeshi linaendelea vizuri na matumizi ya nishati safi ya
kupikia magerezani, huku likitekeleza jukumu la urekebishaji wa wafungwa kwa
ufanisi na kushirikiana na Taasisi mbalimbali za Elimu kama Chuo cha Uhasibu
Arusha (IAA) na VETA na kufanikiwa kutoa vyeti kwa Wafungwa ambavyo
vitawasaidia kuajiriwa na kujiajiri pindi wamalizapo vifungo vyao.
Katika hatua nyingine CGP. Katungu, amewakumbusha Maafisa na Askari kuhusu uwepo wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi Oktoba mwaka huu, na kuwasihi kutumia haki yao ya msingi kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi bora.








No comments:
Post a Comment