MWAKIOJA KUWAWEZESHA WAVUVI KUTUMIA UKANDA WA BAHARI KWA UVUVU WENYE TIJA

Subscribe Us

MWAKIOJA KUWAWEZESHA WAVUVI KUTUMIA UKANDA WA BAHARI KWA UVUVU WENYE TIJA

Ajipanga kujenga kiwanda cha kuchakata Samaki.

Mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Mkinga MMkoa wa Tanga, Twaha Mwakioja.

....................................

Na Mashaka Kibaya, Tanga

TWAHA Mwakioja ni mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Mkinga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni mwanasiasa aliyedhamiria kwa dhati kutumia ukanda wa bahari ya hindi kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za uvuvi wenye tija kwa lengo la kuimarisha uchumi wa wananchi Wilayani humo.

Kuelekea uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani, Mwakioja ameweka bayana baadhi ya vipaumbele vyake pindi wananchi wakimpa ridhaa ya kuiongoza Mkinga akisema, anayo mambo muhimu matatu anavyoamini kuwa yatachangia kuleta mabadiliko chanya kwa jamii.

Miongoni mwa vipaumbele vyake hivyo, Mwakioja amesema, katika kipindi cha miaka mitano atahakikisha Mkinga kunajengwa Kiwanda cha kuchakata mazao bahari, hapa anamaanisha Samaki,ni ili kuongeza ubora huku sekta ya uvuvi ikiongezeka tija.

Mwakioja anasema, ukuaji wa uchumi ni lazima uendane na rasilimali zinazowazunguka wananchi wa eneo husika, hivyo kwa Mkinga ukanda wa bahari utatumika kikamilifu kuwaondolea wananchi umasikini,wengi wao wakiwa wanaojishughulisha na uvuvi.

Kuhusu ujenzi huo wa Kiwanda cha kuchakata samaki, Mwakioja amesema, wavuvi wanapaswa kuendesha shughuli zao kwa tija,ambapo amekusidia kutengeneza ushawishi ndani na nje ya Serikali kuwashirikisha wadau ili kiwanda husika kujengwa.

Huyo ndiyo Twaha Mwakioja mzaliwa wa kitongoji cha Mbuyuni, kijiji na kata ya Man za iliyopo kwenye halmashauri ya wilaya ya Mkinga katika Mkoa wa Tanga,Tanzania.

Mwakioja ni mwenye shahada ya uzamili ya uchumi aliyoipata chuo cha Gothernburg nchini Sweden, pia shahada ya ya takwimu kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam UDSM na  alianza kujishighulisha na Siasa mnamo mwaka 2008.

Dhamira ya Mwakioja ni kuleta mapinduzi makubwa katika kusukuma mbele maendeleo ya watu wa Mkinga, mwanasiasa huyo ameahidi kupita maeneo ambayo Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imepanga kuyafanyia kazi,na hapa mgombea huyo wa ubunge anasisitiza kusema;-

"Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inaelekeza maeneo yote ikiwemo yale ya kiuchumi, kijamii na miundombu".

Aidha Mwakioja anatanabaisha kwamba Mkinga inapaswa kuwa na uchumi unaokwenda kwa kasi, shirikishi na endelevu huku kipato cha mtu mmoja mmoja kikikua, akieleza haja ya wanaMkinga kujiandaa kujenga uchumi wao wenyewe ili kuondokana na umasikini.

Kipaumbele kingine cha Twaha Mwakioja iwapo wanaMkinga watampatia ridhaa ya kuwa mbunge wao ni kuimarisha sekta ya Kilimo, hapa anataja mikorosho,minazi na kwenye ukanda wa milima kuwekwa utaratibu wa kuendeshwa kilimo cha viungo mbalimbali.

Katika sekta hiyo ya kilimo, Mwakioja amesema, ili tija zaidi kupatikana, amekusudia kuwashirikisha wataalam wa kilimo na wadau wengine kuona namna ambavyo nyanja hiyo ambayo ndio uti mgongo wa uchumi itaweza kuimarika.

Zaidi ya yote mgombea huyo wa ubunge amejidhatiti kushirikiana na wadau kuimarisha hali ya masoko ndani na nje ya nchi, ni ili bidhaa zinazozalishwa Mkinga kuuzwa kirahisi na kuleta manufaa kwa jamii husika.

Pamoja na juhudi kubwa za Serikali kuimarisha elimu kwa shoe za msingi,sekondari huku chuo kikuu kampasi ya Mzumbe ikijengwa Mkinga,Mwakioja amesema kwenye eneo hilo atahakikisha wananchi wanaongezewa uwezo ili kuwa tayari kupokea mabadiliko ya kimaendeleo.

"Lazima tubadikishe fikra za wanaMkinga, lengo ni ili kuondokana na fikra za kutothamini maendeleo tuwe na fikra za kusukuma maendeleo kwa kasi ili kukimbia kama maeneo mengine yaliyopo hapa nchini.

Amekiri kwamba, Serikali imeendelea kufanya mambo mengi makubwa na mazuri lakini pamoja na hayo,iwapo wananchi hawatakuwa tayari kukimbiza gurudumu la maendeleo,watashibdwa kwenda na kasi inayohitajika.

Mpango wake mwingine alionao, Mwakioja amesema, ni utunzaji wa mazingira akisisitiza uimarishaji na uboreshaji endelevu, akiwaasa wananchi kutoharibu mazingira ya uganda wa bahari,misitu na ardhi huku akisema kinyume chake ni umasikini wa kudumu.

Kwa mujibu wa Mwakioja, ili Mkinga kupata uchumi imara ni lazima kuwepo na vitu wezeshi, na hapa atawashirikisha wananchi kuitumia vyema teknolojia ya kisasa kuiwezesha wilaya hiyo kujulikana Duniani kote.

"Nitahakikisha tunatumia vyema teknolojia, chochote kizuri kinachopatikana Mkinga kiwepo maeneo mengine na kinachopatikana duniani kipatikane Mkinga"amesema.

Aidha Mwakioja amesema kuwa, atatumia vyema nafasi yake kufanya mazungumzo na Rais mtarajiwa (Dkt Samia) kuhakikisha kwamba,barabara ya kutoka Mabokweni,Daluni hadi Korogwe inafunguka.

Amesema kuwa,kujengwa kwa barabara hiyo kutasaidia ukuaji wa uchumi,watoto watahudhuria masomo vizuri huku ikiwa rahisi kwa usafirishaji likiwemo suala la wajawazito kufika salama kwenye maeneo ya huduma.

Vile vile Mwakioja alisema kuwa maeneo mengine kaka sekta za afya na miundombu mingine itaendelea kufanyiwa kazi kama kawaida lengo likiwa kuharakisha maendeleo.

Katika mahojiano yake hayo na Mwandishi Wetu,Mwakioja hakusita kuzungumzia Uchaguzi wa mwezi Oktoba mwaka huu akisema,Mkinga kutafanyika kampeni za kistaarabu zitakazozingatia sheria ,maelekezo na miongozo kutoka tume ya taifa ya uchaguzi akimaanisha INEC.

Ameeleza kwamba, katika uchaguzi huo, Mkinga wamejipanga kumpatia kura nyingi za kishindo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akiahidi wilaya yake kuwa kinara kwa idadi ya kura za Rais kimkoa.

Twaha Mwakioja akiwa katika moja ya matukio yake ya kikazi na wenzake
Twaha Mwakioja akiwa katika ubora wake wa kukitumikia chama chake cha CCM.
Katibu wa CCM Wilaya ya Mkinga, Stamili Dendego akimkabidhi fomu ya kuwania nafasi ya ubunge, Twaha Mwakioja.
 

Post a Comment

0 Comments