Jina langu ni Anna, msichana mwenye umri wa miaka 20.
Nilipokuwa chuoni mwaka jana, nilikutana na kijana mmoja ambaye alinikonga moyo. Mahusiano yetu yalianza vizuri sana; kila kitu kilionekana kuwa cha ndoto.
Tulikuwa tukizungumza mara kwa mara, tukicheka, tukishirikiana ndoto na mipango ya baadaye.
Hata hivyo, nilikaa katika kile chuo kwa muda wa wiki tatu tu, kisha nikahama kwenda chuo kingine kwa sababu sikuchelewa kugundua kwamba sikukipenda mazingira ya awali.
Nilihisi nitakuwa na amani na maendeleo zaidi nikiwa sehemu mpya. Niliamini kwamba uhusiano wangu na mpenzi wangu hautaathirika na umbali huo, maana nilijua mapenzi ya kweli hupimwa katika kipindi cha changamoto.
Lakini mambo hayakuwa kama nilivyotarajia.
Tangu nilipoingia katika chuo kipya, hali ya mawasiliano ilianza kubadilika.
Mpenzi wangu hakuwahi kunitafuta tena; nilijikuta mimi peke yangu ndiye niliyekuwa na juhudi za kumpigia au kumtumia ujumbe.
Mara nyingine tulikuwa tunapita siku tatu au nne bila kuzungumza, na nilipomuuliza kwanini anafanya hivyo, jibu lake lilikuwa rahisi tu: “niko busy.”
0 Comments