Kwa muda mrefu nilikuwa ninaishi katika mtaa ambao majirani walikuwa wananiwazia mabaya kila siku. Nilipojenga nyumba yangu na kuanza kufanya biashara ndogo ndogo, ghafla nilianza kuona wivu na husuda zikiongezeka.
Walianza kunisema vibaya, kueneza uvumi kuhusu familia yangu na hata mara kadhaa nilikuta vitu vimeharibiwa kwenye shamba langu. Nilihisi nimezidiwa, kwa sababu kila hatua niliyopiga ilionekana kama inawasha moto zaidi wa chuki.
Mambo yalizidi kuwa mabaya wakati nilipopata kandarasi nzuri ya kusambaza bidhaa sokoni. Baadhi ya majirani walijipanga kuhakikisha napoteza mkataba huo. Walianza kunipiga vita hadharani, hata kuwashawishi wateja wasinunue kwangu. Nilishindwa kuelewa kwa nini wanatamani kuona nikishindwa. Nilihisi nimezungukwa na adui kila upande.








No comments:
Post a Comment