Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri mstaafu Wizara ya Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za CCM Jimbo la Ilongero uliofanyika Septemba 3, 2025.
............................................................
Dotto Mwaibale na Philemon Mazalla, Singida
KADA wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) na Waziri mstaafu Wizara ya Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amewahangia
Sh. Milioni 15 wagombea nafasi ya udiwani wa Halmshauri ya Wilaya ya Singida
kupitia CCM kwa ajili ya kampeni za uchaguzi.
Nyalandu alitoa fedha hizo
katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za jimbo jipya la Ilongero lenye kata 21
uliofanyika Septemba 3, 2021.
Akizungumza kwenye uzinduzi
huo aliwataka kila mwananchi kila mwenye kadi ya kupigia kura kujitokeza kwenda
kupiga kura nyingi kwa wagombea wanaotokana na CCM kuanzia za Rais, wabunge na
madiwani.
“Tunahitaji Mkoa wa Singida uwe kinara wa
kura zote katika uchaguzi mkuu na hilo linawezekana kutokana na umoja wetu
tulionao”, alisema Nyalandu huku akishangiliwa.
Aidha, Nyalandu alisema atakuwa bega kwa bega na
mgombea ubunge jimbo la Ilongero, Haiderali Gulamali na kuhakikisha wagombea wa
CCM wanapata kura za kishindo.
“ Nitahakikisha mgombea
wetu wa nafasi ya urais, wabunge na madiwani wanapata kura nyingi jambo la
muhimu kila mmoja wetu siku ya upigaji kura atoke kwenda kushiriki upigaji
nitaungana na timu ya taifa kwenda mikoa yote ndiyo maana kuna basi maalum kwa
kazi hiyo," alisema Nyalandu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata akiwa kwenye uzinduzi huo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ilongero kupitia CCM Haiderali Gulamali akiwa kwenye uzinduzi huo.
Wananchi na Wana CCM wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wagombea udiwani wateule wa Jimbo hilo kupitia CCM wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Basi maalum ambalo lipo chini ya Kada wa CCM Lazaro Nyalandu kwa ajili ya kampeni na kuomba kura za urais za Mgombea urais, wabunge na madiwani likiwa limeegeshwa wakati wa uzinduzi wa kampeni.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri mstaafu Wizara ya Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akisalimiana na wagombea udiwani wa Jimbo la Ilongero.
0 Comments