Siku
hiyo nilikuwa nimeamka mapema kuenda sokoni kununua bidhaa za kuuza dukani
kwangu.
Nilikuwa
nimebeba pesa taslimu kwa sababu wauzaji wengi wa jumla hukubali pesa taslimu
pekee.
Nilipofika sokoni, nilipanga bidhaa
nilizohitaji na kulipa.
Lakini dakika chache baadaye, nilipoingiza mkono mfukoni kuchukua pesa za kulipia mizigo mingine, niligundua mfuko wangu ulikuwa tupu. Nilihisi miguu ikinikatika.








No comments:
Post a Comment