NSSF SINGIDA YAPEWA ELIMU YA DAMU SALAMA, YAWATUNUKU VYETI WANACHAMA WAO - SINGIDANI BLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, 11 October 2025

NSSF SINGIDA YAPEWA ELIMU YA DAMU SALAMA, YAWATUNUKU VYETI WANACHAMA WAO

Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida, Oscar Kalimilwa akizungumza wakati wa kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja Oktoba 10, 2025.

...................................

Na Waandishi Wetu

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Singida limehitimisha Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja kwa kupata elimu ya damu salama kutoka kwa wataalam wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ya Mandewa.

Mtaalam wa Damu Salama kutoka hospitali hiyo, Anyelwisye Philimoni akizungumza wakati wa utoaji elimu hiyo alisema uchangiaji wa damu siyo vita bali inasaidia kuokoa maisha ya watu.

Alisema uchangiaji wa damu hauna madhara yoyote hivyo amewatoa watu waliokuwa na wasiwasi wa kuchangia na kuwataka kujitokeza kuchangia.

“ Mahitaji ya damu katika hospitali zetu ni makubwa mno hivyo inahitajika kwa wingi ili kupunguza changamoto ya upungufu katika Hospitali zetu ya Rufaa, Mkoa na Makiungu,” alisema Philimoni.

Alisema mahitaji hayo yamekuwa yakiongezeka kila siku na kuwa huduma hiyo wamekuwa wakiitoa katika hospitali mbalimbali za binafsi na Serikali na ndiyo maana Serikali imekuwa ikifanya jitihada za kupatikana kwake kwa kuunda timu ya kuitafuta.

Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida, Oscar Kalimilwa akizungumza wakati wa kuhitimisha maadhimisho hayo alisema kwao ni siku muhimu sana kwa kuwakumbuka wanachama wao na kushirikiana nao kwani bila yao wao wasingekuwepo.

Alisema kuwa hivi sasa shirika hilo limepiga hatua kubwa kwani huduma zao zote zinapatikana mkononi kama ilivyo kauli mbiu yao ya mwaka huu isemayo ‘Kidijitali Tumeweza, kwani mwanachama anaweza kufungua madai mwenyewe na mwajiri anaweza kulipa kupitia mfumo huo wa kidijitali.

“Mwanachama anaweza kuona michango yake mwenyewe bila ya kufika kwenye ofisi yetu hii ni hatua kubwa kama shirika tuliyoifikia,” alisema Kalimilwa.

Akizungumza kwa niaba ya waajiri Fr. Constantine Missanga kutoka Hospitali ya Makiungu aliishukuru NSSF kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiwapa na kutambua mchango wao wa kuwachangia wafanyakazi wao.

Katika maadhimisho hayo NSSF Mkoa wa Singida imezitambua taasisi na waajiri wanaojitolea kwa hali na mali kuhakikisha michango ya wanachama wake inawasilishwa kwa wakati na kuwatunuku vyeti maalum wakiwemo watu binafsi ambao ni wanachama wao.

Mtaalam wa Damu Salama kutoka  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ya Mandewa. Anyelwisye Philemoni Kyamba akitoa elimu ya damu salama kwa wafanyakazi wa NSSF Mkoa wa Singida.
Maombi ' Dua' maalum la NSSF likisomwa..
Mwakilishi wa Kiwanda cha Wild Flower, Josephine Peter, akikabidhiwa cheti kwa uchangiaji mzuri kwa wafanyakazi wao.
Fr. Constatine Missanga kutoka Hospitali ya Makiungu akikabidhiwa cheti.
Mkurugenzi (Direct Aid Society) Mkoa wa Singida, Hamisi Ramadhan akikabidhiwa cheti cha uchangiaji mzuri wa wafanyakazi wao.
Wafanyakazi wa NSSF Mkoa wa Singida wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Taswira ya maadhimisho hayo.
Muonekano wa keki maalum ya maadhimisho hayo.
Keki maalum ikikatwa.
Afisa Matekelezo Mwandamizi wa NSSF Singida, Marini Kimario akisisitiza jambo katika maadhimisho hayo.
Wafanyakazi wanaume wa NSSF Singida wakiwa kwenye picha ya pamoja
Picha ya pamoja wafanyakazi wanaume na wanawake katika maadhimisho hayo
Hapa ni mwenydo wa kidijitali ndani ya NSSF.
Ni kudamshi tu kwa kwenda mbele wakati wa kuhitimisha maadhimisho hayo.
Kazi iendelee kwa wafanyakazi wa NSSF Singida mwendo ni wa kidijitali.
Mtaalam kutoka damu salama, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ya Mandewa  Irene Masanja, akimtoa damu Samson Paul wakati akichangia damu.
Mtaalam wa damu salama, Anyelwisye Philemon akimchukua damu mfanyakazi wa NSSF Mkoa wa Singida, Musa Lugendo.

Fuatilia mitandao yetu ya kijamii 

Instagram: @singidaniblog

YouTube: singidani tv online

Tiktok: @singi.daniblog

Contact: +255 754362990

Email: singidani77@gmail.com

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad