Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu ambaye chama chake cha CCM kimemchagua kuwa mgombea wa nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
...................................
Na Dotto Mwaibale, Dodoma
HARUFU ya nafasi ya Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM) inanukia kwa Mbunge wa Jimbo la
Ilala, Mussa Azzan Zungu aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge lililopita la 2020/ 2025 ambaye
ameibuka kinara baada ya kuchaguliwa kwa kura za kutosha kuwa mgombea wa nafasi
hiyo.
Zungu alipata kura 348 katika uchaguzi uliofanyika Novemba 9,
2025, jijini Dodoma na kumshinda
Stephen Masele aliyepata kura 16.
Katika uchaguzi huo Mbunge wa Babati Vijijini Daniel Sillo
aliibuka mshindi kwa kupata kura 362 kwa nafasi ya Naibu Spika.
Uchaguzi rasmi wa Spika na Naibu Spika unatarajiwa kufanyika muda
utakaopangwa kwa kuvishirikisha vyama vingine baada ya kupeleka majina ya
washindi wa nafasi hizo wakiwemo wa CCM walioshinda na kufanya uchaguzi wa
pamoja ili kumpata Spika na Naibu wake.
Wagombea wengine wa nafasi ya Uspika walijiondoa muda mfupi kabla
ya kufanyika kwa uchaguzi huo ambao ni aliyekuwa Spika wa Bunge lililopita Dkt.
Tulia Ackson, Profesa
Paramagamba Kabudi na Mbunge wa Isimani William Lukuvi.
Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo ambaye amechaguliwa na chama chake kuwania nafasi ya Naibu Spika.







No comments:
Post a Comment