Kiongozi wa Kanisa la Ngurumo ya Upako lenye Makao Makuu yake Kisongo mkoani Arusha Nabii Mkuu Dr. GeorDavie, akizungumza.
...............................
Na Dotto
Mwaibale,
HUDUMA ya
Nabii Mkuu, Balozi Dkt. GeorDavie Moses na Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Ngurumo
ya Upako jijini Arusha imetambulika kimataifa baada ya kuteuliwa na Shirika la
Mabalozi wa Amani la Umoja wa Mataifa (UN-PAF) kuwa Mwakilishi na Balozi wa
Afrika Mashariki.
Kutambuliwa
kwa Nabii huyo ambaye ni mlezi wa JMAT Taifa kunatokana na jitihada zake kubwa
anazozifanya za ubalozi wa amani na kusaidia jamii kiuchumi na elimu ambazo
zimekuwa zikionekana si kwa nchi za Afrika Mashariki bali na kimataifa.
Uteuzi huo ulifanyika
Jijini New York Marekani Septemba 9, 2025 ambapo Mwenyekiti wa Dunia wa UN-PAF,
Balozi Kingsley Ossai, alituma barua za utambulisho kwa Serikali ya Tanzania.
Barua hiyo
pia ilitumwa United Nations Chapter ya Tanzania na Ubalozi wa Marekani nchini
kwa ajili ya kumtambulisha Dkt.
GeorDavie katika wadhifa wake huo mpya.
Dkt.GeorDavie amekuwa kioo kwa jamii kwa jinsi anavyojitoa kusaidia makundi
mbalimbali ya watu ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali chini ya Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea
maendeleo na kuwainua wananchi kiuchumi.
Baadhi ya misaada
aliyoitoa hasa katika Mkoa wa Arusha ni Sh. Million
11.5 kwa ajili ya kuwsaidia watu 23 walioathirika na mafuriko yaliyosababishwa
na mvua kubwa mkoani Arusha.
Waathirika wa mafuriko
hayo kila mmoja alipatiwa Sh. 500,000 ambazo zilitolewa kwa ajili ya kununua
chakula, magodoro na vyombo msaada ambao ulikabidhiwa na Balozi wa Nabii huyo
Mtume Sekela Ntondolo.
Msaada mwingine ni Sh.
Milioni 10 alizozitoa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima kiitwacho Faraja
Orphance Children's Home kilichopo maeneo ya Kambi ya Chupa jijini
Arusha.
Aidha Dr. GeorDavie alitoa msaada wa Sh. Milioni 100 kwa
wafanyabiashara wa Soko la Samunge kwa ajili ya kukuza mitaji yao.
Katika matukio mengine Dr. GeorDavie alitoa Sh. Milioni 100 kwa
ajili ya ujenzi wa barabara ya Likamba iliyopo eneo la Kisongo barabara ambayo
iliharibiwa na mvua za masika za mwaka jana.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngorbob, Mohamed Nassoro alisema Nabii
huyo ametumia zaidi ya Sh. Milioni 116.5 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za
kijamii ikiwemo ujenzi wa maabara katika kijiji hicho.
Msaada mwingine alioutoa ni Sh. Milioni 5 kwa ajili ya ununuzi
wa vitanda 20 katika Shule ya Sekondari ya Lepurko iliyopo Halmashauri ya
Wilaya ya Monduli.
Hii ni baadhi tu ya misaada kati ya mingi ambayo ametoa fedha kwa ajili ya kuchangia shughuli za kijamii jambo ambalo ni zuri kwani linachagiza maendeleo ya wananchi.
Chanzo cha Habari hii ni Arusha Digital.








No comments:
Post a Comment