BURIANI MZEE GAMASA MWENDO UMEUMALIZA, UTAKUMBUKWA KWA MENGI KAPUMZIKE KWA AMANI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Monday, 15 December 2025

BURIANI MZEE GAMASA MWENDO UMEUMALIZA, UTAKUMBUKWA KWA MENGI KAPUMZIKE KWA AMANI

Mbunge wa Jimbo la Hanang, Mhe. Asia Halamga, akiwafariji wafiwa. Mwenye koti ni Mtoto wa Marehemu Emmanuel Gamasa.

.................................

Na Dotto Mwaibale

MAJONZI, simanzi na vilio vilitawala wakati wa ibada ya kumuaga Mzee John Gamasa kiongozi mstaafu aliyewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani Hanang’ mkoani Manyara.

Katika mazishi yake viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama cha Mapinduzi, dini, madiwani pamoja na wananchi wa Jimbo la Hanang walihudhuria yakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Hanang, Mhe. Asia Halamga.

Wakati wa uhai wake Mzee Gamasa aliwahi kuhuduma katika chama hicho katika nafasi mbalimbali ikiwemo ya Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Hanang’.

“Mzee Gamasa tutamkumbuka kwa utendaji wake wa kazi alikuwa ni mtu aliyeipenda kazi yake na jinsi alivyokuwa akishirikiana na wenzake hakika ameacha alama,” alisema mmoja wa madiwani. 

Mbunge wa Jimbo la Hanang, Mhe. Asia Halamga,  akizungumza wakati wa mazishi yake  yaliyofanyika Desemba 15, 2025 Kata ya Balang'dalalu alianza kwa kutoa pole kwa  familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki.

” Marehemu John Gamasa alikuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika jamii na taifa kwa ujumla mambo yake yote mema aliyotuachia tutayaendeleza na kuyaenzi,” alisema Mbunge Halamga.

“Tutaendelea kumuenzi mzee wetu John Gamasa kwa kusimamia maadili, hekima na uzalendo alioutamani uendelee kukua katika jamii yetu,” amesema Mhe. Asia Halamga.

Halamga alisema Mzee Gamasa alikuwa msimamizi mzuri wa maadili, mzalendo, mwenye hekima na alikuwa ni rafiki wa kila mtu hivyo wanapaswa kuyaishi maisha yake.

Akizungumza katika mazishi yake Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Mhe. Almishi Hazali, alisema amepokea kwa uchungu taarifa ya kifo cha Mzee Gamasa na kumuelezea kuwa alikuwa mpole, mnyenyekevu, na mpenda amani mambo yaliyofanya apendwe na kila mtu na kuheshimiwa.

Emmanuel Gamasa akizungumza kwa niaba ya familia alitoa shukrani kwa wote walioshiriki katika msiba huo kwa namna moja au nyingine na kueleza hiyo ni ishara ya upendo na mshikamano.

Mbunge wa Jimbo la Hanang, Mhe. Asia Halamga, akiwa na wafiwa..
Mashada yakiwekwa kaburini
Picha zikipigwa mbele ya kaburi la Mzee John Gamasa.
Mazishi ya Mzee Gamasa yakifanyika.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad