KAMBI MAALUM YA UPASUAJI WA MISHIPA YA DAMU YA MOYO ILIYOZIBA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, 12 December 2025

KAMBI MAALUM YA UPASUAJI WA MISHIPA YA DAMU YA MOYO ILIYOZIBA

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inawaomba wataalamu wa afya kutoka Hospitali za Wilaya, Mikoa na Rufaa nchini kuwatuma wagonjwa wenye matatizo ya kuziba kwa mishipa ya damu ya moyo (Coronary Artery Disease) ili wapate huduma za uchunguzi na matibabu katika kambi maalumu ya upasuaji wa mishipa ya damu ya moyo.

Kambi hii itafanyika tarehe 15 hadi 22 Desemba 2025 na itaendeshwa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ushirikiano na wenzao kutoka Hospitali ya Jaslok iliyopo Mumbai nchini India.

Matibabu yatakayotolewa ni pamoja na upasuaji wa kupandikiza mishipa mipya ya damu ya moyo bila kusimamisha moyo (Off – Pump CABG) ili kurejesha mtiririko sahihi wa damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya kuziba kwa mishipa hiyo. Katika kambi hii pia utafanyika upandikizaji wa mishipa mipya ya damu ya moyo kwa wagonjwa wenye mioyo iliyochoka (Low EF) pamoja na matatizo mengine ya afya (Other co morbidities).

Tunawaomba wagonjwa wenye matatizo haya kufika mapema JKCI – Upanga, Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi na maandalizi kabla ya upasuaji.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana kwa simu namba 0716- 696217 Dkt. Alex Joseph, 0657- 761019 Dkt. Sakhiya Yahya, 0737- 000677, 0688-027982 na 0788- 308999 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete."Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu".

 Imetolewa na:


Anna Nkinda

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad