MCHUNGAJI YONA EZEKIELWA KANISA LA MORAVIAN ATOA SOMO KUHUSU MAJILIO - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, December 19, 2025

MCHUNGAJI YONA EZEKIELWA KANISA LA MORAVIAN ATOA SOMO KUHUSU MAJILIO



Mchugaj Yona Ezekiel Kanisa la Moravian Parishi ya Sabasaba (Mandewa) Singida

....................................

Na Dotto Mwaibale
 

MCHUNGAJI Yona Ezekiel Kanisa la Moravian Parishi ya Sabasaba (Mandewa) Singida ahitimisha Kipindi Cha  Majilio kwa kusema yafuatayo  ofisini kwake Kwa njia ya mahojiano

MAJILIO – MAANA YAKE NA UMUHIMU WAKE KWA WAKRISTO

MAJILIO ni Neno la kilatini likiwa na maana ya Advent Kwa maana iyo Kwa tafsiri ya jumla ni wakati wa kuja.

  JAMBO LA KUFAHAMU

Katika kitabu Cha Kiongozi Kalenda ya Kanisa Moravian Tanzania inaonyesha kipindi Cha MAJILIO ni mwaka mpya wa kanisa yaani mwaka. A.ndio maana tunaanza na majilio na hata masomo ya injili hasa siku za ibada ya jumapili yamepangwa Kwa mtiririko unaofuatana

JUMAPILI YA MWISHO KABLA YA MAJILIO

Kwa mujibu wa Kitabu Cha Kiongozi Kalenda jumapili hii inaitwa jumapili ya MFALME KRISTO ANATAWALA. Jumapili hii tayari inaanza kuwaanda wakristo kuanza kipindi cha majilio

YALIYOMO KATIKA KIPINDI CHA MAJILIO

Kwa watu walio wengi wanakuwa na ufahamu kuwa Christmas imekaribia ni kweli kabisa wapo sawa lakini kanisa katika kipindi hiki cha majilio linatafakari hasa juu ya kurudi kwa mara ya pili kwa Bwana wetu Yesu KRISTO hapa tunakumbushwa atakaporudi Kwa mara ya pili

a) Hatakuja Kwa unyonge na udhaifu

b) Atakapokuja kwa mara ya pili atakuja kama muhukumu

c) Atakuja kama mfalme

KIPINDI HIKI WAKRISTO WANATAKIWA KUFANYA NINI?

.Kutafakari mambo yapaswayo kufanya wanaposubiri kurudi kwa mara ya pili kwa Bwana wetu Yesu KRISTO

•Wakristo wanatakiwa kutumia muda mwingi kwa ajili ya maombi na sala maana maombi ni sehemu ya kumsubiri Yesu Kristo anaporudi tena

•Kuendelea kukaa katika neno la Mungu

•Kujilinda na dhuluma,choyo,ugomvi na mambo yote yatakayotufanya kukaa mbali na Mungu

MSHANGAO WA WENGI

Ni kwamba mbona habari ya kurudi kwa Bwana wetu Yesu Kristo imesemwa kwa muda mrefu sana?  nataka niseme mitazamo ya tofauti tofauti toka Kanisa la awali ndio maana tutaona baadhi ya nyaraka za mtume paulo hasa 2WATHESALONIKE 2:1-12 Paulo inaeleza juu ya kurudi kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 

Paulo anawahimiza Wathesalonike kusimama imara, akiwahakikishia kwamba hatimaye Yesu ataiharibu dunia hii kwa pumzi Yake, na kuwafariji walio katika taabu na kwamba hukumu ya Mungu itawashukia waovu, na si watu Wake. 

Kifungu hiki ni wito wa utambuzi dhidi ya mafundisho ya uwongo na ukumbusho wa kubaki waaminifu katikati anaahidi kwamba Bwana Yesu atamwangamiza yule mwasi, na kuleta uharibifu wa haraka kwa wale walioendeleza udanganyifu na kukataa upendo wa Mungu kwa ile kweli.

  LAKINI NI MUHIMU TUFAHAMU ZAIDi

•Siku ya kurudi haijulikani

•Lini atakuja haijulikani

•Twatakiwa kubaki katika hali ya kungoja

kIPINDI CHA KUJIANDAA

Yale yakujiandaa Bwana wetu Yesu krsto ameyafundisha kwa uwazi tena Kwa mifano

1.MFANO WA KWANZA

Wanawali kumi. Mathayo 25:1-13

Kama hiyo mistari ya Mathayo 25 inavyoelezea, kwamba wote walikuwa ni wanawali ikiwa na maana kuwa wote ni wakristo wanaomngojea Bwana. 

Na yale mafuta waliokuwa nayo wote ni “Roho Mtakatifu”. Lakini wengine walionekana kuwa na mafuta ya ziada, na wengine hawana.Hii inafunua aina mbili za wakristo watakaokuwepo siku za mwisho,

AINA YA KWANZA: Hawa ni wale wakristo werevu waliopokea Roho Mtakatifu na kuruhusu Roho wa Mungu kufanya kazi ndani yao kwa kutaka kujifunza na kuendelea kupokea mafunuo zaidi ya Roho wa Mungu mpaka kufikia cheo cha utimilifu Kristo (Waefeso 4:13), mtu wa dizaini hii kila siku anakuwa tayari kujifunza jambo jipya, hivyo anahama kutoka utukufu hadi utukufu kila siku kiu na bidii ya kuendelea kumjua Mungu

AINA YA PILI: Hawa ni wale wakristo waliojilegeza na kujisahau ambao walishapokea Roho Mtakatifu (ambayo ndio yale mafuta kwenye taa zao) lakini sasa baada ya kupokea Roho wa Mungu WANAMZIMISHA ndani kwa kutomruhusu tena aendelee kuwafundisha mambo mapya, na kuwatoa hatua moja ya kiroho hadi nyingine. Kwasababu kumbuka kazi ya Roho Mtakatifu ni kutuongoza katika kuijua kweli yote,

2.MFANO WA PILi

Bwana aliyesafiri na kurudi kutaka taarifa kwa watumishi wake

Mathayo 25:14-30

3.MFANO WA TATU

Siku atakayogawa kondoo na Mbuzi

Mathayo 25:31-46

WAPENDWA ni muhimu kufahamu kuwa maisha ya kila siku ni majilio ya kugonja na kusubili dumuni katika wema na mema ili atakapokuja atukute tupo tayari

                            MWANAKONDOO AMESHINDA " 

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad