Dkt. Japhet Zephania Ngamba
.....................................
Na Onesmo Kapinga, Dar es Salaam.DAKTARI bingwa anayetibu kwa dawa za asili, Japhet Zephania Ngamba amesema amefanikiwa kuwatibu watu wengi wenye waliovunjika viungo vya mwili, ikiwamo mbavu na nyonga.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ngamba ambaye anafanyia shughuli zake Chanika, Kata ya Zingiziwa, Ilala, alisema amekuwa akitibu watu waliovunjika uti wa mgongo, miguu na sehemu nyingine za mwili na mifupa kuweza kuunga kwa muda wiki mbili.
Ngamba alisema baadhi ya watu waliosaidiwa ni wale ambao walishindikana kupona kwa muda mrefu wakitokea Hospitali mbalimbali za jijini Dar es Salaam.
Daktari huyo alisema anatumia majani ya miti shamba katika kuwatibu watu waliovunjika viungo vya mwili.
Alisema kazi hiyo ambayo ameifanya kwa zaidi ya miaka 12, anatumia utalaamu wake kwa kumpepea kwa upepo mtu aliyepata kadhia kwa kutumia majani ya miti shamba.
"Nimesaidia watu wengi walioshindikana kupona hospitali baada ya kuvunjika mbavu, mkono, nyonga wakija kwangu nawatibu na mifupa inaunga kwa muda wa wiki mbili tu," alisema Ngamba.
Pia alisema kutokana na tiba yake hiyo amekuwa akipokea zaidi ya watu 12 kila siku wenye changamoto ya mifupa.
Daktari huyo alisema mtu yeyote mwenye shida ya kuvunjia mifupa akipata matibabu yake atakuwa na uhakika wa kupona ndani ya wiki mbili.
Helena Zakaria ambaye ni Mama Lishe mkazi wa Chanika Kimwani Mtaa wa Barakoa ametoa ushuhuda wa kupona mguu wake uliovunjika baada ya kupata matibabu kwa Dkt. Ngamba.
"Nikiwa katika kazi yangu ya mama lishe niliteleza kuvunja mfupa wa kidole changu cha mguuni ambapo nilinunua dawa za kutliza maumivu na siku iliyofuata mguu ulivimba sikuweza kusimama kutokana na maumivu makali ndipo nilipokwenda kwa Dkt. Ngamba (Ngosha) ambaye alinitibu kwa wiki mbili na kupona kabisa," alisema Helena.
Helena alisema Daktari huyo amesaidia watu wengi waliopata changamoto ya kuvunjika na baadhi yao walikuja wakitoka maeneo mbalimbali ya Tanzania ikiwamo Mkoa wa Ruvuma.
Selemani Yusuph mkazi wa Chanika naye alisema alipona baada ya kuvunjika kidole cha mguuni baada ya kutibiwa na Dkt. Ngamba.
Dkt. Ngamba amesema anafanya kazi hiyo kwa kufuata taratibu za nchi.
Jitihada ya kumpata Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Tanzania (TAHPC), Profesa Japhet Otieno ili kuzungumzia kama wanamtambua Dkt. Ngamba kwa huduma anayoitoa kwa wananchi hazikuweza kufanikiwa baada ya kupigiwa simu mara kadhaa bila ya kupokelewa.
Kwa mahitaji ya huduma ya Dkt. Ngamba unaweza kuwasiliana naye kwa namba ya simu namba 0767333970.







No comments:
Post a Comment