Viongozi wa Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) ambayo kwa sasa inasimamiwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na mashine mbili mpya za kisasa za usingizi na ganzi zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 115 zitakazotumika kwa wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji katika hospitali hiyo. Mashine hizo zimetolewa msaada na na Shirika la Global Health Ministry (GHM) la nchini Marekani.
Afisa mauzo wa kampuni ya Heyer ya nchini Ujerumani, Michael Mchagi akimuelekeza daktari wa upasuaji wa Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) Emmanuel Lema jinsi mashine ya usingizi na ganzi inavyounganishwa. Shirika la Global Health Ministry (GHM) la nchini Marekani limetoa msaada wa mashine mbili za kisasa za usingizi na ganzi zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 115 zitakazotumika kwa wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji katika Hospitali hiyo ambayo inasimamiwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Mchungaji wa kiroho wa Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) ambayo kwa sasa inasimamiwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Godwin Lekashu akiweka wakfu mashine mbili mpya za kisasa za usingizi na ganzi zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 115 zitakazotumika kwa wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji katika hospitali hiyo. Mashine hizo zimetolewa msaada na na Shirika la Global Health Ministry (GMH) la nchini Marekani.
Muonekano wa mashine mbili mpya za kisasa za usingizi na ganzi zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 115 zilizotolewa msaada na Shirika la Global Health Ministry (GMH) la nchini Marekani ambazo zitatumika katika hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) ambayo kwa sasa inasimamiwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).







No comments:
Post a Comment