Wanawake wakiondoka na watoto wao kwa kutumia viti mwendo vilivyo tolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara, Mhe. Regina Ndege.
..............................
Na Dotto Mwaibale
KUJITOA kusaidia watu wengine ni jambo jema ambalo
linakubalika na hata vitabu vitakatifu vya dini vimezungumzia suala hilo.
Tumekuwa tukiona au kusikia jamii ikiaswa kujenga utamaduni wa kua
na moyo wa kujitolea kusaidia watu wenye uhitaji haswa
Watoto yatima, wanaoishi katika mazingira magumu na makundi mengine.
Kutoa ni moyo wa mtu na wala siyo utajiri lakini pia inaweza kuwa ni wajibu wa kila mmoja wetu kujitoa kuwasaidia watu wenye
mahitaji ili kupata baraka za Mungu.
Tabia ya kutoa inalinda na kuheshimu utu wa mtu kwa kumpatia chakula, malazi, mavazi, huduma za afya, upendo, amani na mahitaji mengine ya kibinadamu ambayo yanadumisha mshikamano miongoni mwa jamii.
Watu wengi ambao wanajitoa kusaidia jamii kazi
yao inakuwa imenyooka na wanajiamini.
Leo napenda nimzungumzie Regina
Ndege Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mbunge huyu ni mtu wa watu, anayejitoa bila ya kuchoka kusaidia makundi mbalimbali ya watu wenye
uhitaji sambamba na shughuli nyingine za maendeleo.
Mbunge Ndege amekuwa akifanya kazi zake kwa bidii kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Manyara, hasa katika masuala ya maendeleo na ustawi wa
jamii.
Kwa nyakati tofauti ametoa msaada wa viti mwendo kwa watoto
ambapo aliwahi kutoa viti hivyo kwa watoto watatu walemavu wa Wilaya ya Mbulu,
ili kuwasaidia kwenda shule.
Ambapo pia Januari 11, 2026 ametoa tena viti mwendo kwa
watoto 10.
Jambo hilo siyo dogo na linafanywa na viongozi wachache kama Mbunge Ndege.
Kutokana na kuwiwa kwake kuwatumikia wananchi amekuwa
akiwahimiza wanawake wa Mkoa wa Manyara
kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimia 10 ya wanawake, vijana na walemavu
inayotolewa na Halmashauri mbalimbali nchini kutokana na mapato ya ndani yenye
malengo ya kuwakwamua kiuchumi.
Katika kupambana na mazingira na kumuondoa mwanamke katika
matumizi ya kuni na kuingia katika matumizi ya nishati safi aligawa majiko
ya ya gesi kwa wanawake na wanaume Mama
na Baba lishe wa mji mdogo wa Magugu wilayani Babati mkoani humo.
Mbunge Ndege katika kusaidia shughuli nyingine za maendeleo
alitoa mifuko 100 ya saruji na matofali 200 kwa ajili ya kuchangia mradi wa
ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), wilaya zote za
mkoa huo.
Jambo lingine kubwa alilolifanya ni la kuiomba serikali
kufanya tathmini ya kina ili kukabiliana na athari za maporomoko na mafuriko
katika Mkoa wa Manyara.
Hayo ni baadhi tu ya mambo machache kati ya mengi
aliyoyafanya mbunge huyo katika mkoa huo na tunategemea mambo mengi makubwa yanakuja
kutoka kwake baada ya kutetea tena nafasi yake hiyo ya ubunge wa Viti Maalum
Mkoa wa Manyara kwa kipindi cha pili.
Kutokana na jitihada yake kubwa anayoifanya ya kuunga mkono kazi kubwa anayoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea wananchi maendeleo Januari 11, 2026 Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA), Kanda ya Kaskazini chini ya Katibu wake Ezekiel Tlanka walimtunuku hati ya shukrani kutokana na mchango wake uliofanikisha kikao cha Jumuiya hiyo kilichofanyika Desemba 23, 2025.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Ndege, akiwa amembeba mtoto wakati wa hafla ya kutoa msaada wa viti mwendo kwa watoto wenye mahitaji maalumu Januari 11, 2026.
Viongozi wa Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) wakimkabidhi hati ya shukrani Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara MMhe. Regina Ndege.
Makala hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990.







No comments:
Post a Comment