PSPTB INAVYOSIMAMIA VIWANGO VYA KITAALAMU KATIKA MANUNUZI NA UGAVI NCHINI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, January 17, 2026

PSPTB INAVYOSIMAMIA VIWANGO VYA KITAALAMU KATIKA MANUNUZI NA UGAVI NCHINI

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi mkoani Singida Januari 15, 2026.
..........................
 Na Dotto Mwaibale, Singida

Manunuzi na Ugavi ni  Kitengo kilichoanzishwa kwa lengo la kuleta ufanisi na kutoa huduma kwenye masuala ya manunuzi, utunzaji na usambazaji wa bidhaa na huduma mbalimbali ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kwenye ngazi ya mkoa kinaongozwa na Afisa Ugavi Mkuu ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.

Serikali kwa kutambua umuhimu wa kitengo hicho ilianzisha Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kwa ajili ya kusimamia viwango vya kitaalamu na maadili ya wataalamu katika nyanja za manunuzi na vifaa.

Katika kutekeleza na kukamilisha jukumu hilo, sheria ya kuanzishwa kwa bodi hiyo imeipa mamlaka PSPTB kutayarisha na kuishauri serikali juu ya sera na yanayohusiana na taaluma ya manunuzi na vifaa.

Kupanga, moja kwa moja, kuratibu, kufuatilia na kudhibiti wafanyakazi mahitaji katika manunuzi na vifaa na usimamizi wa taaluma.

Mambo mengine yanayofanywa na bodi hiyo ni kutoa ushauri wa kitaalamu kwa kutambua nakutoa mafunzo kwa taasisi zote za ndani ya nchi sadaka kozi katika manunuzi na vifaa na huduma za ushauri katika manunuzi na usimamizi vifaa , vifaa vya utunzaji, usambazaji, ufungaji, usimamizi wa kitaalamu, menejimenti ya mikataba na udalali.

Kuunda, kuanzisha na kutekeleza matengenezo ya viwango vya maadili na kusimamia shughuli za wataalamu wa manunuzi, vifaa vya wataalamu, wakaguzi manunuzi, vifaa na wakaguzi hisa, mafundi manunuzi na vifaa mafundi na mazoezi ya taaluma ya manunuzi na usimamizi vifaa ;Kutoa mafunzo au kutoa fursa kwa ajili ya mafunzo ya watu katika kanuni; taratibu na mbinu ya manunuzi na usimamizi vifaa.

Kuendesha mitihani ya kitaaluma na na tuzo nyingine ya bodi katika manunuzi na vifaa, ukaguzi wa manunuzi, vifaa na hisa ukaguzi na masomo mengine yanayohusiana na manunuzi na usimamizi vifaa.

Kufanya usajili wa wataalamu wa manunuzi na vifaa, kuweka na kudumisha madaftari ya usajili wa wataalamu wa manunuzi na vifaa kwa mujibu wa PSPTB na kutathmini sifa za kitaaluma na vitendo kwa lengo la usajili wa watu chini ya bodi hiyo.

Halikadharika majukumu mengine ya bodi hiyo ni kudhamini, kupanga na kutoa vifaa kwa ajili ya mikutano, semina, mijadala na mashauriano juu ya masuala yanayohusiana na manunuzi na vifaa vya usimamizi na kuagiza ada inayolipwa kwa bodi ili kusaidia wanachama wa umma katika suala hilo.

Kwa muktadha huo kila mwaka wafanyakazi wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wamekuwa wakifanya kikao cha baraza la wafanyakazi kwa ajili ya kupanga mikakati kabambe ya kuboresha utendaji kazi.

Januari 15-16, 2026 wafanyakazi wa bodi hiyo wamekutana mkoani Singida kwa ajili ya kuweka mikakati ya pamoja namna ya kujadili utendaji wa kazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua kikao hicho alisema watakuwepo mkoani Singida kwa ajili ya kujadili mpango kazi wa kitaasisi pamoja na kufanya tathimini ya utendaji ya mwaka uliopita na kuweka mkakati wa pamoja wamaboresho katika idara mbalimbali na vitengo.

“Tunafanya kikao hiki ili tuweze kuendana na sheria inayotuongoza kutekeleza majukumu yetu mbalimbali ya Serikali,” alisema Mbanyi.

Mbanyi alisema baraza hilo la wafanyakazi huwa linafanyika mara mbili na ni chombo cha kiuwakilishi na kuwa katika kikao hicho kuna wakuu wa idara na vitengo vyote na kila kitengo kimetoa mwakilishi mmoja mmoja wa kusikiliza na kuwasilisha mijadala ambayo wataona inafaa kwa maboresho ya utendaji katika maeneo yao.

Alisema katika taasisi za Serikali mabaraza hayo ya wafanyakazi yapo kwa mujibu wa sheria ya mahusiano kazini na katika usimamizi wa ujumla wa kitaifa wapo chini ya ofisi ya waziri mkuu.

“Katika kikao hiki tutajadili utendaji wa nusu mwaka katika mwaka huu wa fedha wa 2025/ 2026 tuangalie tumefanya nini wakati tukijielekeza mwaka mpya wa fedha wa 2026/2027 na kuangalia maboresho zaidi na kuona tunaendaje,” alisema Mbanyi.

Alisema katika kikao hicho pia watasikiliza maoni ya wafanyakazi ambao hawapo kwenye vikao vya maamuzi na kuyapeleka kwenye vikao vya menejimenti kwa ajili ya kuyafanyia kazi.

Kwa upande Mwenyekiti  wa  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), Tawi la  Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Dodoma, Shilla Mwandu alisema ushirikiano mzuri baina ya bodi hiyo na Tughe umeimarisha utendaji kazi kwa watumishi.

“ Ushirikiano uliojengeka kwa muda mrefu baina ya TUGHE na PSPTB umeongeza utendaji wa wafanyakazi kutokana na kuzitatua changamoto zao mahali pa kazi,” alisema Mwandu.

Alisema TUGHE waliingia mkataba na bodi hiyo tangu mwaka 2006 ambapo wamedumisha demokrasia ambayo imeimarisha uhusiano wao na utendaji kazi na shughuli za taasisi hiyo.

Alisema chama hicho kimekuwa mkono wa mwajiri pamoja na Serikali katika kutetea na kuimarisha mahusiano na taasisi hiyo.

Mwandu alisema chama hicho tangu kimeanza wenyeviti wao wamebadilishana kwa awamu mbili na kumekuwa na demokrasia ya kusikiliza maoni ya wafanyakazi na kufanya majukumu ya utendaji kufanyika kama yalivyopangwa.

Alisema mshikamano huo baina ya uongozi wa chama hicho na mwajiri  haujawa tofauti na yeyote zaidi ya kuwaunganisha kama watumishi wa umma.

Mwandu alitoa rai kwa taasisi nyingine za umma ziwe na mabaraza ya wafanyakazi  ambayo yatasaidia kuwawezesha wafanyakazi kustawi kimasilahi na mambo mengine baada ya chama hicho kuchukua maombi yao na kuyapeleka Serikali na kufanyiwa kazi.

Msimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala PSPTB, Nancy Mwamakimbula alisema kupitia baraza hilo wanategemea kupata maoni mengi ya wafanyakazi ya kuboresha utendaji wa kazi.

Alisema katika baraza hilo pia watazungumzia masuala ya bajeti na maoteo ya bajeti ya mwaka ujao wa 2026/ 2027 pamoja na utekelezaji wake.

“Kimsingi tunatarajia baraza hili kuwa na manufaa sana kwetu hasa katika maboresho ya utendaji kazi na kuboresha mambo yote ambayo watumishi wote watatamani yaboreshwe yanayohusu taasisi na taaluma ya Ununuzi na Ugavi nchini.Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi mkoani Singida Januari 15, 2026.Mwenyekiti  wa  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), Tawi La PSPTB-Dodoma. Shilla Mwandu akizungumza. Afisa Rasilimali  Watu na Utawala PSPTB, Nancy  Mwamakimbula akizungumzaWafanyakazi wa PSPTB wakishiriki kikao hicho

Picha ya pamoja baada ya kufunguliwa kikao hicho

Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad