Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ambayo Tanzania imeshinda kuwa eneo bora la Utalii wa Safari Duniani (World’s Leading Safari Destination) kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji, Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar tarehe 05 Januari, 2026. Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) yenye Makao Makuu yake Jijini London, Uingereza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha Tuzo ambayo Hifadhi ya
Serengeti imeshinda kuwa Hifadhi bora Duniani (World’s Leading
National Park, Ikulu ndogo ya Tunguu
Zanzibar tarehe 05 Januari, 2026. Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya World
Travel Awards (WTA) yenye Makao Makuu yake Jijini London, Uingereza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Wizara ya
Maliasili na Utalii kabla ya kukabidhiwa Tuzo tatu ambazo Tanzania imeshinda
katika Utalii, Afrika na Duniani. Kikao hicho kilifanyika Ikulu ndogo ya
Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Januari, 2026. Tuzo hizo zimetolewa na Taasisi ya
World Travel Awards (WTA) yenye Makao Makuu yake Jijini London, Uingereza.
Muonekano wa Tuzo tatu za “WORLD TRAVEL AWARDS”ambazo Tanzania
imeshinda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan
Chande mara baada ya kupokea Tuzo 3 za Utalii za “WORLD TRAVEL AWARDS” ambazo
Tanzania imeshinda, Ikulu Ndogo Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Januari, 2026.













No comments:
Post a Comment