RAIS SAMIA AOMBWA KUNUSURU MGOGORO WA ARDHI KANISA LA KIKRISTO - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Tuesday, 6 January 2026

RAIS SAMIA AOMBWA KUNUSURU MGOGORO WA ARDHI KANISA LA KIKRISTO

 Mchungaji wa Kanisa la Kristo, David Mathias

....................................

Na Mwandishi Wetu. 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa kuingilia kati mgogoro wa ardhi unaendelea dhidi ya Kanisa la Kristo Temeke na baadhi ya watu waliovamia eneo la wazi mbele ya kanisa hilo. 

Ombi hilo kwa Rais Dk. Samia limetolewa na Mchungaji wa kanisa, David Mathias, baada ya kumalizika kwa misa ya ibada iliyofanyika Jumapili.

Mchungaji Mathias alisema kuwa amechukua uamuzi wa kumwomba Rais DK Samia kuingilia kati mgogoro huo wa ardhi uliodumu zaidi ya miaka 15, baada ya watendaji wake ngazi ya chini kushindwa kuutatua.

Alisema kwa miaka mingi sasa waumini wa kanisa hilo, wanakosa Uhuru wa kuabudu kutokana kelele za magari yanayopaki katika eneo hilo lililovamiwa na baadhi wa watu hao. 

Mchungaji Mathias alisema wakati wa ibada waumini wake wanashindwa kuabudu kwa heshima kutokana na kero wanayoipata, kwani wakati mwingine sauti za honi za magari inaingiliana na ibada.           

Pia alisema wakati mwingine waumini wao wanashindwa kupita na kuingia ndani ya kanisa kutokana na magari mengi ambayo anakuwa yamepati katika eneo hilo.  

Mchungaji Mathias alisema wakati kanisa hilo, linajengwa 1963 eneo lilikuwa la wazi, hivyo  uvamizi  huo  unaathiri shughuli za uendeshaji wa kanisa hilo. 

"Tumekuwa katika eneo hili kwa miaka mingi na tunalimiliki kwa mujibu wa sheria," alisema Mchungaji Mathias.

Naye, Katibu wa kanisa hilo, Nicolaus Kamwagila, alisema kanisa limekuwa katika kadhia ya muda mrefu na kuiomba serikali ya ngazi ya juu chini ya Rais Dk. Samia kuingilia kati ili kunusuru mgogoro huo.

Kamwagila alisema Rais DK. Samia anatakiwa kutembea na kauli mbinu ya "kazi na utu" na utu huo  usishushwe thamani yake. 

Alisema kauli mbiu hiyo ya Rais Dk Samia inatakiwa kufanya kazi kwa kuliangalia kanisa la  kristo Temeke, ambalo linaangalia kutafuta haki kutokana eneo hilo kuvamiwa na baadhi ya wananchi wanaolitumia kwa ajili ya kupaki magari.

Katibu huyo alisema anaamini Rais Dk. Samia atasikiliza kilio chao cha muda mrefu kutokana na mgogoro huo. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad