MBIVU NA MBICHI MKUTANO WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI 2026 - DODOMA - SINGIDANI BLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, 12 February 2026

MBIVU NA MBICHI MKUTANO WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI 2026 - DODOMA

 Meneja wa Huduma za Utangazaji, Mhandisi Andrew Kisaka akitoa wasilisho lilohusu Matokeo na Utekelezaji wa Mapendekezo yatokayo na Utafiti wa Huduma za Utangazaji Nchini katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji 2026 Februari 12, 2026 Jijini Dodoma.

................................................. 

Na Dotto Mwaibale, Dodoma 


MKUTANO Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji 2026 umeanza rasmi kwa mawasilisho yaliyowasilishwa na wawasilishaji wabobezi katika Ukumbi wa Mikutano wa New Generation Jijini Dodoma huku ukitoa mwanga wa utatuzi wa baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta hiyo.


 Akifungua mkutano huo Naibu Waziri  Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Hamis Mwinjuma alisema Serikali imesikia na kuzitatua changamoto za muda mrefu ikiwemo kupunguza ada za usajili ili kuwezesha vyombo vingi kuwa na usajili na kutoa Habari zenye tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla


Alisema usajili wa blog ada ya kuomba ni Sh. 1O,000 na ada ya mwaka itakuwa Sh. 50,000.


Kwa upande wa Wazalishaji maudhui ya online (You Tuber) ada ni Sh. 100,000 huku ada ya maombi ikiwa ni Sh.20,000.  


Miongoni mwa washiriki wa mkutano huo ni vyombo vya utangazaji ambavyo ni televisheni, redio na mitandao ya kijamii.


Mawasilisho yaliyowasilishwa yalikuwa matatu la kwanza likiwa ni Matokeo na Utekelezaji wa Mapendekezo yatokanayo na utafiti wa Huduma za Utangazaji Nchini yaliyo wasilishwa na Mhandisi Andrew Kisaka kutoka TCRA.


Wasilisho la pili lilikuwa ni Fursa na Faida za Uwekezaji wa Teknolojia katika Utangazaji vijijini, lililowasilishwa na Zuhura Selemani ambaye ni Mhadhiri Msaidizi.


Wasilisho la tatu lilihusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Huduma za Utangazaji  wa Redio Vijijini (Uzoefu wa UNESCO), lililowasilishwa na Mhadhiri Dk. Egbert Mkoko kwa niaba ya Nancy Mwaisaka kutoka UNESCO. 


 Mkutano huo wa siku mbili ambao umeanza leo Februari 12, 2026 Jijini Dodoma utafikia tamati kesho Februari 13, 2026 na umeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa habari nchini.Mhadhiri Msaidizi Zuhura Selemani akitoa Wasilisho Kuhusu Fursa na Faida za Uwekezaji wa Teknolojia katika Utangazaji Vijijini.Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.Mkutano ukiendelea.Wadau wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.

Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo
Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanahabari Kusini Mwa Africa (MISA-TAN), Elizabeth Riziki akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mkutano ukuiendelea.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile na Mtendaji Mkuu wa Baraza hilo, William Shao wakiwa kwenye mkutano huo.
Waandishi wa Mitandao ya Kijamii (Blogers) wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Programu Manager wa Kisaco Media, Emile Mwaipopo, Mkurugenzi wa Madelemo News, Lilian Madelemo na Miga picha wa Kujitegemea, Swaum Said.
Wamiliki wa Blogs wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Othman Maudi Mwendeshaji wa Blog ya Zanzibar News, Mr. Verbs Mkurugenzi Mtendaji wa Habarika24 Blog,  na Cathebat Kajuna Mwendeshaji wa Blog ya Kajunason.
Mtangazaji Nguli, Abdallah Majura akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa P-FM Radio ya Jijini Dodoma, Erick Mutahaba akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 
Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad