MLALI: TUMEMALIZA MGOGORO WA ARDHI PUGU KINYAMWEZI - SINGIDANI BLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, 14 February 2026

MLALI: TUMEMALIZA MGOGORO WA ARDHI PUGU KINYAMWEZI

 
 Wanawake wa Mtaa wa Kinyamwezi Kata ya Pugu wakifurahia baada ya eneo la kuzikia lilodaiwa kuvamiwa kurejeshewa baada ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Fahad Mlali kufuatilia mgogoro huo na kushinda.
...............................
 
Na Mwandishi Wetu 
 
 MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa Kinyamwezi, Kata ya Pugu, Ilala, jijini Dar es Salaam, Fahad Mlali, amesema kwamba amefanikiwa kumaliza kero ya muda mrefu baada ya kurudisha eneo la kuzikia kwa wananchi. 
 
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa wananchi uliofanyika jana,  Pugu Kinyamwezi, Mlali alisema kwamba eneo hilo, ambalo linadaiwa kuvamiwa na mkazi mmoja Elizabeth Mwakapangala, iilitengwa na Halmashauri ya Ilala kwa ajili ya shughuli za mazishi.
 
Mlali alisema kwamba baada ya kufuatilia uhalali wa umiliki wa eneo hilo, alibaini ni mali ya Pugu Kinyamwezi na wananchi waliojenga kwa ajili  ya makazi wanatakiwa kubomoa nyumba zao na kuondoka. 
 
."Ninafuraha sana, ndugu wananchi utata wa eneo hili ambalo lipo Pugu Kinyamwezi limepata ufumbuzi," alisema Mlali. 
 
Mwenyekiti huyo, alisema kwamba wananchi aliojenga katika eneo lililotengwa kwa ajili ya shughuli za mazishi wanatakiwa kuanza kubomoa nyumba zao na kutoa bati kidogo kidogo kabla ya greda 'tingatinga' halijafika.
 
Pia alisema kwamba wananchi wake wanatakiwa kuendeleza kuzika katika eneo hilo, kwani ramani inasomeka liko Pugu na sio Kata ya Buyuni, Ilala. 
 
Mlali alisema kwamba ataendelea kuwapambania wananchi kwa kila jambo ili kuhakikisha anatibu kero zao. 
 
Alisema kwamba baada ya kumaliza utata uliogubikwa katika eneo hilo lililotengwa kwa ajili ya shughuli za mazishi wananchi wake wanatakiwa kuishi kwa amani na utulivu. 
 
"Nawashukuru sana wananchi kwa kushirikiana kwa pamoja na leo (juzi), ukweli umejulikana eneo hill la kuzikia ni la kwetu," alisema Mlali.
 
 Awali, Elizabeth alidai eneo hilo ni mali yake na aliamua kukata viwanja na kuwauzia wananchi baada kushinda kesi iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu ya Ardhi Tanzania.
 
Washtakiwa katika kesi hiyo, alikuwa Mwanasheria wa Serikali, Mkurugenzi wa Halmashauri wa Ilala na Mamlaka ya Viwanja wa Ndege (TAAA), ambao washindwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad