Je, usaliti ukigonga moyo wa mwanamke, je, kuna kitu hubaki sawa? Machozi ya usiku, maswali yasiyo na majibu na picha zinazozunguka kichwani kila saa. Hiyo ndiyo hali aliyopitia Lucy wa mjini Eldoret baada ya kugundua mumewe alikuwa na uhusiano wa pembeni kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Lucy alikuwa mke mwenye kujituma. Alilea watoto wao wawili, akasimamia biashara ndogo ya familia na kuhakikisha nyumba iko sawa. Hakuwahi kufikiria angekuja kusimama mbele ya ushahidi wa usaliti wa wazi.
Siku moja alipokuwa akitumia simu ya mumewe kupiga picha, ujumbe wa kimapenzi uliingia. Ujumbe mmoja ukafuata mwingine. Ukweli ukawa wazi.
Maumivu na Hasira Zilizomkaba
Lucy alihisi dunia imesimama. Alitaka kuondoka mara moja. Alitaka kuwaambia wazazi wake na hata kupeleka kesi mahakamani. Lakini ndani yake kulikuwa na sauti ya kumtaka atulie.








No comments:
Post a Comment