Jina langu ni Bakari, mkazi wa jijini Tanga. Kwa miaka mingi, maisha yangu yamekuwa simulizi la kusikitisha linapokuja suala la mahusiano. Kila nilipokuwa nikijipanga kuoa na kuanza taratibu za kutoa posa, mambo yalikuwa yakiharibika ghafla bila sababu ya msingi. Mara mwanamke anabadilika tabia, mara tunagombana kwa jambo dogo, au anapotea kabisa kwenye maisha yangu.
Umri ulienda hadi nikafika miaka 42 nikiwa bado sijaingia ndani na mwanamke. Maumivu makali zaidi yalikuwa yanatoka kwa marafiki zangu wa karibu. Kila tukikutana, mazungumzo yalikuwa kuhusu watoto wao wanavyokua na shule wanazosoma. Nilibaki kuwa mtazamaji, na wakati mwingine walikuwa wananikebehi kwa kuniita “bachelor sugu” au kunifananisha na kijana mdogo anayeanza maisha. Shinikizo la familia na jamii lilinipelekea kukosa amani na kujifungia ndani mara nyingi.








No comments:
Post a Comment