RC TANGA: ZIARA YA WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU IWE CHACHU YA KUHAMASISHA UWEKEZAJI - SINGIDANI BLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, 15 February 2026

RC TANGA: ZIARA YA WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU IWE CHACHU YA KUHAMASISHA UWEKEZAJI


Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dr. Batilda Buriani 

............................... 
 Na Hamida Kamchalla, MKINGA.

KUPITIA ujio wa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dkt. Batilda Buriani ameomba iwe chachu ya kuendelea kuhamasisha wawekezaji kwenda mkoani humo ili kuufungua kiuchumi.

Dkt. Buriani ameyasema hayo leo Februari 15 wilayani Mkinga wakati Waziri Mkuu akikagua Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi ya Tanga, na kwamba maeneo mengi yanayozunguka vyuo vikuu yamefungua biashara na kukua kiuchumi.

"Chuoni hapa tutahitaji maduka, huduma za kibenki, hivyo ni fursa kubwa sana na ujio wako utafungua uwekezaji mkubwa na hivyo mapato yataongezeka, mwaka 2021 Halmashauri ya Mkinga waliokuwa wanakusanya mapato Shilingi Bilioni 1.2, lakini sasa wanakusanya Bilioni 2.9,

"Mapato hayo yamepatikana chuo hiki bado hakijaanza,tuna imani kubwa baada ya kuanza mapato yataongezeka zaidi kupitia uwekezaji huu unaofanywa na Serikali," aalisema.

Amesema Wilaya ya Mkinga ina fursa kubwa katika kilimo, utalii, uchumi wa buluu, mazingira pamoja na madini ambayo hayapatikani mahali popote katika Mkoa wa Tanga zaidi ya Wilaya hiyo.

Katika kilimo, amesema wilaya hiyo linalimwa zao la korosho ambalo awali lilikuwa linapelekwa nchi jirani kwa ajili ya soko lakini kwasasa wizara imeanzisha mnada wa kuuza korosho kupitia stakabadhi ghalani.

"Tumefurahishwa sana na mafunzo ambayo wenzetu wa Chuo cha Mzumbe wanayafundisha kwani wamegusa zaidi vijana wa Wilaya ya Mkinga kutokana na fursa zilizopo" amebainisha.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad