UDSM, TCRA KUANZA MAHOJIANO UTAFITI WA HADHIRA YA WASIKILIZAJI - SINGIDANI BLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, 13 February 2026

UDSM, TCRA KUANZA MAHOJIANO UTAFITI WA HADHIRA YA WASIKILIZAJI

 Mhadhiri wa Chuo Kikuu chaa Dar es Salaam Dr. Egbert Mkoko akitoa wasilisho katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji, lililohusu  utafiti utakaofanywa na chuo hicho kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ili kujua idadi ya watu wanaoangalia maudhui kwenye vyombo vya utangazaji.

.................................... 

Na Dotto Mwaibale, Dodoma.

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), waanza rasmi kufanya utafiti wa hadhira ya wasikilizaji wa radio, watazamaji na wafuatiliaaji wa maudhui ya majukwaa ya kidijitali.

Hayo yamebainishwa na Mhadhiri wa chuo hicho Egbert Mkoko wakati akiwasililisha wasilisho lililohusu  utafiti utakaofanywa ili kujua idadi ya watu wanaoangalia maudhui kwenye vyombo vya utangazaji kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji 2026 ulioandaliwa na TCRA.

Dr. Mkoko alisema utafiti huo utafuata miongozo ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na kuwa  utaanza Februari 15, 2026 kwa kuzungumza ana kwa ana na wadau.

Alisema utafiti huo kwa upande wa radio watafanyiwa mahojiano watu 51, televisheni watu 14 na mitandao ya kijamii watu 57.

Alisema vyombo vya habari vitakavyofikiwa ni  radio, televisheni, Cable TV na online.

Dr. Mkoko alisema utafiti huo utagusa maeneo mbalimbali kama vile kujua idadi ya watu ambao wanaangalia maudhui kwa wingi na vyombo gani vya utangazaji ambavyo vinapendwa zaidi.

Alitaja mambo mengine ni maudhui gani zaidi yanayopendelewa na watizamaji kati ya ndani na nje ya nchi na namna maudhui yanavyozingatia watu wenye mahitaji maalumu.

Aidha, alitaja jambo lingine kuwa ni watangazaji wa matangazo wanapendelea kuyatoa kwenye vyombo gani na uzingatiaji wa maudhui ya watoto.

Dr. Mkoko alisema mahojiano hayo ya ana kwa ana na makundi hayo ambayo yataanza Februari 15, 2026 yatafikia tamati Machi 30, 2026.

Meneja Miradi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Wilfred Charles akiwasilisha wasilisho linalohusu nafasi ya mfuko huo katika kuwezesha Utangazaji Vijijini.
Watangazaji wakongwe wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Abdallah Majura, Penzi Mnyangumi, Edda Sanga na Jane Paul Mailleh aliyekuwa Msaidizi wa Edda Sanga.. 
Wadau wa habari wakiwa kwenye mkutano huo ambao unafikia tamati leo Februari 13, 2026.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano huo ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Waendeshaji wa Blogu wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mwendeshaji wa Malunde1, Frank Wandiba Mwendeshaji wa Blog ya Harakati za Jiji na  Mkurugenzi wa Kwanza Blog, Athumaaani Shomari.
Mablogers wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mapuli Misalaba Mkurugenzi wa Misalaba Media, Stella Herman kutoka SI Media na Neema Nkumbi kutoka Udadisi Live Blog.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mhariri na Mmiliki wa Mzalendo News Blog, Zena Mohamed Mwandishi wa habari Nyemo FM.
Mabloger wakiwajibika na kujadiliana jambo kwenye mkutano huo.
Mabloger wakiwajibika na kujadiliana jambo kwenye mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad