WASIFU WA MWANAHABARI NGULI ULIMBOKA BENJAMIN MWAKILILI, MWENDO UMEUMALIZA KAPUMZIKE KWA AMANI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, February 20, 2026

WASIFU WA MWANAHABARI NGULI ULIMBOKA BENJAMIN MWAKILILI, MWENDO UMEUMALIZA KAPUMZIKE KWA AMANI

ULIMBOKA BENJAMIN MWAKILILI
Kuz: 29/11/1958
Kuf: 18/02/2026

Kusoma:

Shule ya msingi: IYELA, Shule ya Secondary : Mbeya Secondary School 
 
Marehemu alijiunga na Chuo cha Anga Tanzania Visiwani (ZANZIBAR) 

Kazi:
Akiwa Zanzibar marehem alifanikiwa kuanza kazi ya kuongoza ndege.(Air Traffic Controller)

Baadae alihamishiwa Tanzania Bara Mkoa wa Dar es Salaam katika kitengo hichohicho cha Air Traffic Controller.
 
Marehemu alifanya kazi ya Anga kwa kipindi cha miaka(5)

Baadae aliingia Sekta ya Habari
 
Marehemu alijiunga na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya (Mbeya Press Club) na baadaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Mbeya Press Club nafasi iliyomuwezesha kuwa mjumbe wa UTPC (Union of Tanzania Press Club)- Umoja wa Waandishi wa Habari Tanzania,
Akiwa Mjumbe wa UTPC, Mwaka 2000  aligombea Udiwani Kata ya IYELA kupitia Chama cha CCM na kushinda ambapo aliongoza kwa kipindi cha miaka 5 (2000_2005)

Mwaka 2002 kipindi akiwa diwani, aliwania  Urais wa UTPC Ngazi ya Taifa na kushinda kiti cha Urais wa Umoja wa klabu za Waadishi wa Habari Tanzania na kuongoza kwa kipindi cha miaka 5 (2002_2007)

Baada ya hapo alijiunga na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania( Tanzania Redcross Society) ambapo baadae alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mbeya..
 
katika nyazifa ya uenyekiti aliteuliwa katika nafasi mbalimbali kwa nyakati tofauti  
A. Aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maafa na Majanga Mkoa wa Mbeya
B. Aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Dharura Uwanja wa Ndege cha Kimataifawa  Songwe.

C. Aliteuliwa kuwa Mjumbe wa NEC (kamati Kuu ya Taifa ya Tanzania Redcross Society).
 
Katika nafasi hiyo ya Mwenyekiti Mkoa, aliweza kushika nafasi kadhaa katika ngazi ya taifa ikiwepo kuiwakilisha nchi katika mikutano ya Kimataifa katika chi za France, Switzerland na AUSTRALIA 
pamoja na nchi za Africa South africa na Kenya.

Hadi kufika mwaka 2019, marehemu alitunukiwa uanachama wa maisha kwa kupewa Nishani tatu (3)(GOLD, BRONZE, SILVER)

Aidha katika uhai wake Marehemu aliweza kuanzisha Chuo cha Afya na Tiba (Faraja Helath and Management (Faraja HEMA) Chuo ambacho kilijikita katika Uuguzi Usaidizi, na mafunzo ya huduma ya kwanza.

Pia aliweza kuanzisha Zahanati  (FARAJA DISPENSARY)
Katika kipindi hichohicho aliweza kufungua Chuo cha AFRSACO (African Safar College) kilichosajiliwa chini ya NACTE, ambacho kilikuwa kikitoa kozi za Computer, Secretary and Tour Guide ambapo alikua akitoa kipaumbele kwa wahitimu wa daraza la saba  ili kuendana na kasi ya kiutandawazi.

Mwaka 2023, aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Tulia Trust.

Mwishoni mwa mwaka 2023,aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika Mkoa wa Mbeya.

 Enzi za Uhai wake Ulimboka Benjamin Mwakilili.

Mazishi yake yanatarajia kufanyika kesho Jumamosi Februari 21, 2026 nyumbani kwake Igawilo Uyole Jijini Mbeya. Vita vya maisha umepigana, Mwendo umeumaliza kampumzike kwa amani. Bwana alitoa na Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe milele daima.

Imeandaliwa na Dotto Mwaibale 0754362990
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad