.................................
Na Hamida Kamchalla, Tanga.
WAZIRI Mkuu Dr. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwasili kesho (13/2) mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya siku nne (4), kufuatilia, kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo pamoja na kuongea na wananchi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dr. Batilda Buriani, Waziri Mkuu atapokelewa wilayani Handeni eneo la Mkata majira ya saa tatu asubuhi akitokea Mkoa wa Pwani.
Dr. Buriani amesema miradi ipatayo iiliyogarimu zaidi ya shilingi Bilioni 700 tatembelewa ambapo katika Wilaya ya Handeni atakagua mradi mkubwa wa umeme ambao utasaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa Wilaya za Pangani, Muheza na Korogwe lakini pia atazindua chumba cha wa gonjwa mahututi na kuweka jiwe la msingi.
Katika Wilaya ya Kilindi, Waziri atakagua mradi wa tenki la maji na baada ya hapo atakwenda kukagua hospitali ya Wilaya ya Kilindi na kuweka jiwe la msingi na kuelekea wilayani Korogwe ambapo atakagua mradi mkubwa wa miji 28.
Amesema Februari 15, Waziri ataeleke Wilaya ya Mkinga na kukagua ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na kuweka jiwe la msingi na siku hiyo hiyo atakwenda Tanga jiji na kukagua Bandari ya Tanga pamoja na kuongea na wananchi katika viwanja vya CCM Wilaya (Lamore).
Februari 16, ataelekea Wilaya ya Mkinga na kukagua mradi mkubwa wa Bomba la mafuta Ghafi (EACOP) pamoja na matenki ya kuhifadhia mafuta, lakini pia atatembelea kukagua kiwanda cha kutengenezea mifuko.
Baada ya hapo ataelekea Wilaya ya Pangani na kukagua daraja la mto Pangani na atatoa maelekezi baada ya kupata taarifa ya ujenzi huo na baadaye ataelekea Wilaya ya Muheza ambapo atakagua jengo la halmashauri.
Katika Wilaya ya Lushoto atakagua na kuweka jiwe la msingi katika hoteli kubwa inayotambulika Kidunia ambapo siku ya Februari 17 atatembelea Hospitali ya Wilaya ya Lushoto katika kituo cha kutengenezea Oxygen ambapo atakagua na kuzindua kituo hicho.
Msafara huo utaondoka kuelekea Mlalo na kukagua shule mpya ya Amali na baada ya hapo kutakuwa na majumuisho ya Mkoa kabla ya msafara wake kuelekea mkoni Kilimanjaro









No comments:
Post a Comment