Ni nani amewahi kusikia mwizi akirudisha gari mwenyewe na kuomba
msamaha? Hilo ndilo lililotokea kwa Caroline, mfanyabiashara wa nguo kutoka
Nairobi, ambaye aliamka asubuhi moja na kukuta gari lake halipo maegesho. Lakini
ndani ya saa ishirini na nne, simu zilianza kuingia kwa njia iliyowaacha wengi
wakiwa hawaamini.
Caroline alikuwa amerudi nyumbani usiku akiwa amechoka. Alipaki
gari nje ya geti kama kawaida. Asubuhi alipotoka kuwapeleka watoto shule,
alikuta maegesho yapo wazi. Alidhani labda mumewe alikuwa amelichukua. Lakini
simu ilipothibitisha kuwa hakuna aliyejua lilipo, hofu ilianza kupanda.
Gari lile halikuwa tu chombo cha usafiri, lilikuwa sehemu ya biashara yake. Alilitumia kusambaza bidhaa kwa wateja wake.








No comments:
Post a Comment