Awafikia wafungwa Gereza la Kiomboi Wilaya ya Iramba.
Mwenyekiti wa Ramadhan Charity Programme, Ahmed Misanga (katikati), akikabidhi chakula na vitu vingine kwa ajili ya futari kwa wafungu Waislamu waliofunga waliopo Gereza la Kiomboi Wilaya ya Iramba mkoani Singida Machi 12, 2026.
....................................
Na Dotto Mwaibale, Singida
WAISLAM kote Duniani wapo kwenye mfungo wa Mwezi mtukufu wa
Ramadhani ambao ni mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu, unaochukuliwa kuwa
na umuhimu mkubwa wa kiroho.
Mwezi huo ni kipindi cha saumu ya kila siku kutoka alfajiri
hadi jioni, kujitolea, ibada, na kurudi kwa Mwenyezi Mungu na n i maalum kwa
sababu Qur'ani iliteremshwa ndani yake na inazingatiwa kama nguzo ya nne ya
Uislamu.
Umuhimu wa Ramadhani ni wa kufunga, kujizuia na kula,
kunywa, na mambo ya anasa kuanzia alfajiri hadi magharibi, ikiwa ni sehemu ya nguzo
Tano za Uislamu.
Mwezi wa Qur'ani ni mwezi ambapo Qur'ani iliteremshwa kama
uongofu kwa watu, hivyo kuimarisha uhusiano na kitabu hicho.
Mwezi huo ni ukuaji wa Kiroho na ni wakati wa kutafakari, kujiboresha kiroho, na
kuongeza juhudi katika ibada na kufuata mafundisho ya Uislamu na kuongeza
huruma na nidhamu na kuwa Saumu inasaidia kusitawisha nidhamu, huruma, na
ukaribu zaidi na Mwenyezi Mungu.
Kimsingi, Ramadhani ni muda wa kusafisha nafsi, kuomba
msamaha, na kuimarisha imani.
Faida kumi na umuhimu wa Kufunga Ramadhani katika Uislamu
ambapo imetafsiriwa Ramadhani ni mwezi wa umuhimu mkubwa wa kiroho kwa Waislamu
ulimwenguni kote, unaoadhimishwa na mfungo wa kila siku kutoka alfajiri hadi
jioni.
Tumeona katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
watu mbalimbali wakijipatia Thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kutokana na
kufuturisha wenzao walio na Swawm na kupata Thawabu pasipo kupungukiwa na kitu.
Jambo hilo la kufuturisha linaweza kufanywa na Mwislaam yeyote
kutokana na chochote atakachojaaliwa na Mwenyezi Mungu na wala siyo mpaka awe
tajiri hata tende tu mbele ya Mwenyezi Mungu zinatosha kabisa.
Nimeanza kuzungumzia umuhimu wa mwezi huo na thawabu
wanazopata wanaojitoa na kufuturisha wenzao nikimkusudia Ahmed Misanga ambaye
ni Mwenyekiti wa Ramadhan Charity Programme.
Misanga kila mwaka katika kipindi kama hiki cha Mwenzi
Mtukufu wa Ramadhani amekuwa akitoa chakula na misaada mingine katika maeneo
mbalimbali nchini jambo ambalo linampa thawabu kubwa mbele ya Mwenyenyezi
Mungu.
Katika kutimiza moja ya nguzo katika dini ya kiislam jana Machi
12, 2026, amefika katika Gereza la Wilaya Iramba ( KIOMBOI), na kutoa Sadaka ya IFTAR kwa ajili ya
wafungwa Waisilamu waliofunga Mwezi
Mtukufu wa Ramadhani.
Misanga ameonesha upendo kwa tendo hilo kwani wahenga
wanasema kutoa ni moyo na wala siyo utajiri.
Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990.








No comments:
Post a Comment