Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dkt. Khamis Said 'kushoto', akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mwalimu Dkt. Alexius Revocatus Kagunze, alipotunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) katika Ustawi wa Jamii na Uongozi wa Biashara kutoka Christian Ministerial Training University (CMTU) ya nchini Zambia katika hafla iliyofanyika Februari 28, 2026 Mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Greeling Global Peace Organization na mmiliki wa CMTU, Profesa Askofu Kennedy Songwe.
...............................
Na Dotto Mwaibale, Shinyanga
NAIBU Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dkt. Khamis Said, amesema kwamba amani ni nguzo kuu ya maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni Duniani.
Dkt. Said ambaye alikuwa mgeni rasmi ameyasema hayo Februari 28, 2026, mkoani Shinyanga katika maadhimisho ya Siku ya Amani na Upendo Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani humo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wanaharakati wa amani na wageni kutoka ndani na nje ya nchi.
Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), yalifanyika sanjari na hafla ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) katika Ustawi wa Jamii na Uongozi wa Biashara kutoka Christian Ministerial Training University (CMTU) cha nchini Zambia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mwalimu Alexius Revocatus Kagunze.
Dkt. Said alisema kuwa UNESCO ilianzishwa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia kwa lengo la kujenga utamaduni wa amani kupitia elimu, sayansi na utamaduni, ili kuzuia migogoro na kuhakikisha dunia inabaki katika mshikamano wa kudumu.
“Tunampongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga kwa uteuzi wake wa kuwa Balozi wa Amani. Hii ni ishara kuwa viongozi wa ngazi zote wana wajibu wa kueneza ujumbe wa amani, uvumilivu na mshikamano wa kitaifa,” alisema Dkt. Said.
Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dkt. Khamis Said, akihutubia kwenye maadhimisho hayoMwalimu Dkt. Kagunze akionesha cheti alichokabidhiwa.Wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kushoto ni Profesa Stephano Nzowa wa African Graduate Universit, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dkt. Khamis Said na Mwenyekiti Mwanzilishi wa Greeling Global Peace Organization na mmiliki wa CMTU, Profesa Askofu Kennedy Songwe.Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dkt. Khamis Said (katikati) akiwa na viongozi mbaaalimbali meza kuu.Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dkt. Khamis Said, akiwasalimia washiriki wa maadhimisho ya siku ya aamani duniani mkoani Shinyanga.Mwimbaji wa nyimbo za injili Nesta Sanga akimvika beji maalumu Edelfrida Stephen Tibaija, Afisa Program Tume ya Taifa ya UNESCO. (kushoto), katika maadhimisho hayo.






No comments:
Post a Comment